SEMFUKO AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA WANYAMAPORI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

SEMFUKO AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA WANYAMAPORI.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini - TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa za ufugaji wa wanyamapori zinazopatikana katika Taasisi ya TAWA.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
14 Jul 2024
SEMFUKO AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA WANYAMAPORI.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini - TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa za ufugaji wa wanyamapori zinazopatikana katika Taasisi ya TAWA.

Ameyasema hayo Julai 13, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Katika Maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa ambayo kwa Mwaka 2024 leo yamefikia tamati.

"Sehemu kama Afrika ya Kusini ufugaji wa wanyamapori ni mkubwa sana, kwahiyo mimi natoa rai kwa wananchi hasa watanzania kuingia katika biashara hiyo ya ufugaji wa wanyamapori" amesema.

Aidha Meja Jenarali (Mstaafu) Semfuko amesema ili watanzania waweze kupata kitoweo cha nyamapori kwa urahisi wanapaswa kuingia katika biashara ya ufugaji wa wanyamapori na kwakufanya hivyo wataziwezesha bucha za wanyamapori kufanya kazi vizuri.

Sambamba na hilo, Semfuko amesema TAWA ina mipango mingi ya kuhakikisha  inapata wawekezaji wakubwa na wadogo ili wawekeze katika maeneo mbalimbali inayoyasimamia kama vile kuwekeza katika mahoteli, vitalu vya uwindaji wa kitalii na ranchi za wanyamapori ili kuongeza idadi ya wanyama hao.

Maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yenye kauli mbiu "Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji" yalianza Juni 28, 2024 na kuzinduliwa  rasmi Julai 03, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi ambapo leo Julai 13, 2024 yamefungwa na Mhe. Dr. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI

SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA NANENANE

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA NANENANE

WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

TANZANIA YAUNGA MKONO AGENDA ZA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI NA USALAMA WA MAENEO YA UTALII.

TANZANIA YAUNGA MKONO AGENDA ZA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI NA USALAMA WA MAENEO YA UTALII.