SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI

Serikali imesema uhamisho unaoendelea wa wananchi waishio ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni wa hiari baada ya wananchi husika kupewa Elimu, kuhamasika na kuridhia wenyewe kwenda Msomera na maeneo mengine waliochagua kupisha uhifadhi wa raslimali kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo siyo utalii.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
01 Aug 2024
SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI

Serikali imesema uhamisho unaoendelea wa wananchi waishio ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni wa hiari baada ya wananchi husika kupewa Elimu, kuhamasika na kuridhia wenyewe kwenda Msomera na maeneo mengine waliochagua kupisha uhifadhi wa raslimali kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo siyo utalii. 

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyapori nchini, Dkt. Alex Lobora amefafanuakwamba kuhama kwa  hiari kwa wananchi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kunatokana na tathmini shirikishi iliyofanyika mwaka 2020 na siyo  upotoshwaji unaoenezwa  na baadhi ya  vikundi vya watu wenye nia ovu. 

 “Tathmini hiyo ilionesha kuwa shughuli za kibinadamu zinazoendelea ndani ya eneo hilo siyo rafiki kwa maisha ya binadamu na ni hatarishi kwa binadamu wenyewe na uhifadhi.” Amesisitiza Dkt. Lobora 

Ameongeza kuwa pamoja na kutokuwa na mazingira rafiki kwa maisha na maendeleo ya binadamu, eneo la Ngorongoro limehifadhiwa kwa sheria Sura Na.284 ambayo hairuhusu baadhi ya maendelezo kwa mustakabali wa kulinda na kuhifadhi maliasili na malikale zilizomo katika eneo hilo ambazo siyo tu ni muhimu kwa Tanzania bali dunia nzima  na kwamba eneohilo ni  la urithi wa dunia.

Kuhusu madai ya baadhi ya wananchi hususan wamasai kuwa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni eneo lao la mababu (ancestral land) na kwamba wao ni watu wa asili (indigenous people) wa eneo hilo hayana msingi wowote na ni upotoshaji wa ukweli na unaolenga kuwatofautisha wananchi wa eneo hilo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye nia njema kwa watu wake.  

Ameeleza kuwa katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro yapo makabila mengine kama  Wadzabe na wadatoga ambao walitangulia kuishi NCA kabla hata  ya jamii ya Wamasai.

“Kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Sehemu ya 15 na 17 vinatoa uhuru wa watu na uhuru wa kuwa mahali popote na hakuna ubaguzi chini ya Sehemu ya 13 ya Katiba. Tanzania haina watu wa asili bali watu wote ni sawa na wanaruhusiwa kuishi mahali popote ilimradi wasivunje Sheria. Aidha, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya Mwaka 1999 inafafanua kuwa Tanzania ina aina tatu tu za ardhi (Ardhi Iliyohifadhiwa, Ardhi ya Kijiji na Ardhi ya Jumla). Hakuna “ancestral land”. Amesisitiza Dkt. Lobora

Amefafanua kuwa yako madhara mengi kwa wananchi waishio ndani ya NCA ambayo yanawafanya kupingana na “Millennium Goals” zinazoeleza hali inayotakiwa kwa mtu anayetakiwa kuitwa binadamu ikiwemo kukosa haki ya kumiliki ardhi na kukosa huduma nyingine za msingi ambazo haziwezi kupatikana ndani ya eneo lililohifadhiwa kwa mujibu wa Sheria. 

Aidha amesema wananchi wanaohamia Msomera na maeneo mengi kwa hiari wananufaika na mambo mengi wanayopatiwa  na serikali ambapo ametaja baadhi ya mambo hayo kuwa  ni pamoja na kupewa fidia ya maendelezo na motisha ikiwa ni hatua ya Serikali kuwaokoa kutoka kwenye maisha duni yasiyo na matumaini na kuboresha maisha yao.

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA NANENANE

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA NANENANE

WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

TANZANIA YAUNGA MKONO AGENDA ZA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI NA USALAMA WA MAENEO YA UTALII.

TANZANIA YAUNGA MKONO AGENDA ZA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI NA USALAMA WA MAENEO YA UTALII.

UNDERSTANDING THE REASONS BEHIND THE VOLUNTARY RESETTLEMENT OF NGORONGORO RESIDENTS WITHIN THE RESERVE.

UNDERSTANDING THE REASONS BEHIND THE VOLUNTARY RESETTLEMENT OF NGORONGORO RESIDENTS WITHIN THE RESERVE.