TTCL KUPELEKA HUDUMA ZAKE NCHI JIRANI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

TTCL KUPELEKA HUDUMA ZAKE NCHI JIRANI.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL) limesema linampango wa kuhakikisha linaendelea na mchakato wa kufikisha huduma zake nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
12 Jul 2024
TTCL KUPELEKA HUDUMA ZAKE NCHI JIRANI.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL)  limesema linampango wa kuhakikisha linaendelea na mchakato wa kufikisha huduma zake nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. 

Akizungumza leo Julai 12,2024 jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 kimataifa ya Biashara maarufu ,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya TTCL(T-PESA),Lulu Mkudde wakati akiongea na waandishi wa habari,amesema mpaka sasa huduma hiyo imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi,Rwanda,Zambia na Malawi. 

"Tunaposema tunafungua milango ya kidigitali inamaanisha kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa watu wengine,"amesema na kuongeza 

"Mpaka sasa shirika limefanya mambo mbalimbali ikiwemo huduma  ya TTCL - Pesa ambapo katika Sabasaba hii tumekuja na huduma ya Akaunti Pepe inamuwezesha mteja kufungua akaunti yake bila hitaji ,mteja anauwezo wa kutumia akaunti yake saa 24 kwa siku,"amesema.

Amesema mpaka sasa,Shirika  limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo  zaidi ya wilaya 98 zikiwa nazo zimefikishiwa Mkongo wa mawasiliano.

Mkudde amesema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha juhudi za huduma za Elimu, Afya na Maendeleo ya kiuchumi ambayo  yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

"Niwahakikishie TTCL ,itahakikisha huduma za mawasiliano inakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali za kujipatia shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato kupitia fursa hii ya Interneti kwa gharama nafuu,"amesema

Akizungumzia Huduma ya T-cafe,Mkudde amesema huduma ya T -CafĂ©  ni huduma ya WiFi  ambayo ina waondolea  adha wafanyabiashara, waandishi wa habari na wataalamu wa masuala ya ushauri katika kufanya kazi zao wakiwa nje ya ofisi.

Amesema ni huduma ambayo inasaidia mtu yoyote  kufanya kazi nje ya ofisi kwa kupata  uwezo wa kutumia huduma zao  katika kutekeleza huduma zake .

"Shirika limeanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wote kufanya shughuli zao kwa haraka na gharama nafuu,ambapo  kwa  kipindi hiki cha Sabasaba  tumeshuhudia huduma hii  inavyofanya kazi kwa speedi ya hali ya juu na wananchi kwa wakati wote walikuwa wakitumia   katika maonesho hayo,"amesema.

Aidha amesema kupitia  maonesho haya,TTCL imepata  fursa ya kutoa elimu na kujenga uelewa kwa wananchi  kuhusu huduma hiyo wanayoitoa  ambayo inamfikia  mwananchi moja kwa moja .

"Tumepokea maombi mengi wateja wanahitaji huduma hii kwani yameleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifurushi vya kawaida ambavyo shirika limeleta huduma hii kumuwezesha mwananchi kutumia Internet bila kikomo,"amesema.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.

PPAA YAOKOA BILIONI 567.6 KATIKA MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA

PPAA YAOKOA BILIONI 567.6 KATIKA MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA