Mwenyekiti wa bodi ya T Pesa kutoka Shirika mawasiliano Tanzania TTCL Richard Mayongela ametoa rai kwa wananchi kutumia huduma zinazozalishwa nchini ili kuchochea maendeleo lakini kukuza uchumi wa Taifa.
Wito huo ameutoa leo jijijni Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane Nzuguni wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL lililopo kwenye maoneshe hayo.
Amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika shirika hilo umepelekea kuwepo na huduma bora zinazotolewa na shirika kwa umma.
"Wito wangu kwa watanzania na wadau tutumie vilivyo vyetu nyumbani kumenoga TTCL ni shirika la umma kwa hiyo wanapolitumia tunarejesha faida kwa wananchi wenyewe",Amesema.
Amesema kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika sasa hivi wamepeleka huduma ya internet kwenye majengo ya serikali lakini pia huduma ya fiber Mlangoni sasa inapatikana ambapo mteja anapelekewa huduma hiyo mpaka kwenye makazi yake.
Aidha ameongeza kuwa TTCL imeendelea kusambaza huduma za mawasiliano katika vyuo na taasisi mbalimbali za umma.
"Tunashukuru serikali kwa uwekezaji mkubwa ambao umeufanya kwa miaka ya hivi karibuni sasa shirika linaweza kuwafikia wateja kwenye nyanja mbalimbali ambapo sasa hivi tumeanza kwenye kilimo na biashara",amesema.
Akizungumzia huduma ya lipa kwa mkupuo amesema shirika limekuja na huduma hiyo kwa madhumuni ya kurahisisha malipo kwa wakulima,wafanyabiashara na wadau mbalimbali ambao wanahitaji kuwalipa watu wengi.
"Shirika limekuja na huduma hii kwa madhumuni ya kurahisisha malipo badala ya mtu kubeba pesa na kumlipa mtu mmoja mmoja sasa unaweza kulipa wote kwa mkupuo",Amesema.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO
DAR CITY YAING’ARISHA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU AFRIKA MASHARIKI
Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano katika tukio la kariakoo.