

MRAJISI wa vyama vya ushirika nchini Dkt Benson Ndiege ameipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kuanzisha huduma ya malipo kwa mkupuo kwa vyama vya ushirika.
Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho ya Wakulima Nanenane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma amesema huduma hiyo imekuja wakati muafaka na itakuwa mkombozi kwa wakulima nchini.
"Kwenye vyama vya ushirika tuna vyama vya ushirika vya kilimo,kifedha madini vya mifugo na maeneo mengine yote kwa hiyo huduma hiyo itakuwa na tija kubwa",Amesema.
Amesema kwenye vyama vya ushirika kuna watu zaidi ya 500 ambao wanalima zao linalofanana hivyo wanapohitaji kulipana njia ya malipo ya mkupuo itawasaidia zaidi.
"Mfumo huu unaenda kuwasaidia vyama vyote vya ushirika kwani ni njia salama na ya kuaminika na itasaidia katika utendaji kazi",Amesema.
Aidha Dkt Ndiege ameongeza kuwa kutokana na umuhimu wa huduma hiyo wanapanga kukutana na uongozi wa TTCL na kuangalia jinsi huduma hiyo itakavyoenda kuwanufaisha vyama vya ushirika nchini.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.