Vifungashio vya madini kuboreshwa kudhibiti utoroshaji. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

Vifungashio vya madini kuboreshwa kudhibiti utoroshaji.

TUME ya madini ipo kwenye mchakato wa kuboresha vifungashio vya madini katika masoko ya madini nchi nzima ikiwa ni mkakati wa kuendelea kudhibiti utoroshaji wa madini.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
11 Jul 2024
Vifungashio vya madini kuboreshwa kudhibiti utoroshaji.

TUME ya madini ipo kwenye mchakato wa kuboresha vifungashio vya madini katika masoko ya madini nchi nzima ikiwa ni mkakati wa kuendelea kudhibiti utoroshaji wa madini.

Hayo yamesemwa na Aloyce Bwana Mteknolojia Maabara katika Maonesho ya 48 Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema, mkakati wa Tume kuanzia mwaka huu wa fedha 2024/2025 ni kuhakikisha vifungashio katika masoko yote ya madini vinakuwa vya aina moja tofauti na ilivyo sasa vinatofautiana.

Amesema,  kuwa na aina moja ya vifungashio itapunguza utoroshaji wa madini unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu na kuinyima Serikali mapato.

“Kuwa na vifungashio vya aina moja itasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini,  masoko ya madini yamesaidia  kupunguza utoroshaji wa madini kwa kiasi kikubwa lakini kama  Tume ya Madini tutaendelea kuchukua hatua madhubuti kudhibiti  zaidi utoroshaji wa madini, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi,”amesema.

Naye, Baiton Mtebe Mjiolojia  akizungumzia masoko ya madini amesema masoko yalianzishwa kama njia mojawapo ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata soko la uhakika la madini yao baada ya kuchimba,  Serikali kupata mapato na takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na wachimbaji wadogo wa madini, kuuza madini kulingana na bei elekezi inayotolewa na Tume ya Madini kulingana na soko la dunia. Vilevile kudhibiti utoroshaji wa madini kwa wachimbaji na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Amesema  mpaka sasa Tume ya Madini ina masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini 102 nchini ambayo yameongeza mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye mapato kutoka asilimia tano hadi asilimia 40 Mwaka 2022/2023.

Amesisitiza kuwa masoko ya madini yamepunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya utoroshaji wa madini pamoja na kuleta ushindani kwa wafanyabiashara wa madini kupitia masoko na vituo vya ununuzi wa madini.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.

PPAA YAOKOA BILIONI 567.6 KATIKA MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA

PPAA YAOKOA BILIONI 567.6 KATIKA MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA