WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango zanzibar zimeendelea kuimarisha ushirikano wake kupitia njia mbalimbali ikiwemo michezo

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
30 Mar 2024
WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango zanzibar zimeendelea kuimarisha ushirikano wake kupitia njia mbalimbali ikiwemo michezo.

Akizungumza katika Bonanza la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Kilimani jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, amesema michezo hiyo ni moja kati ya njia moja wapo ya kudumisha muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Tupo hapa Kilimani kama wanamichezo kwa maana ya Ofisi ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na wenzetu Ofisi ya Rais, wizara ya fedha kule Zanzibar, kila mwaka wakati wa Pasaka huwa tunakutana kama watumishi na kama wanamichezo kwa ajili ya kufanya Tamasha la Pasaka ambapo tunakuwa na michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, netiboli pia, kubwa sana katika mashindano haya ni ushirikiano kati ya sisi tuliopo Tanzania Bara na wenzetu walioko Tanzania Zanzibar’’ Alisema Bw. Mwenda.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Utumishi na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Suleiman Mohammed Rashid, mara baada ya kufungua Bonanza hilo, Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, ameshukuru Uongozi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara kwa kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar kuimarisha uhusiano kupitia Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka.

‘’Tunashirikiana katika masuala ya michezo kama haya kwa ajili ya kuimarisha udugu wetu na kuzidi kufahamiana katika masuala ya kazi, kwahiyo ni kitu kizuri ambacho tunakiendeleza tumekirithi kutoka kwa watangulizi wetu na kina manufaa makubwa sana kwetu sisi tunawashukuru viongozi wetu wa Wizara zetu hizi mbili kwa kuendelea kuimarisha mahusiano haya na yanatusaidia kwa kiasi kikubwa’’ alisema Bw. Uweje.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka ambaye pia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa, alisema kwa mwaka huu Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo   imefanya maboresho katika Bonanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma hususani katika mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kuweka timu mbalimbali za nje mbali na timu ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.

‘’Tukiongelea histori ya nyuma wakati huu tumeboresha kidogo, kwa sababu kawaida tulikuwa tukicheza sisi Hazina Bara na Hazina visiwani lakini leo tumekuwa na timu sita’’ aliongeza Bw. musifa.

Tamasha hili la Pasaka limekuwa likifanyika kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na limekuwa likifanyika kwa kuunganisha pande zote mbili za Muungano kwa miaka yote hiyo. Na timu zilizoshiriki ni pamoja na timu ya Maveterani kutoka Bara na visiwani,Police FC, Hazina Sports club, GPSA, PSPTB, Area C na nyingine zao.

 

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC