ONANA AKIRI KIWANGO CHAKE KUSHUKA ALIPOTUA MAN UNITED | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

ONANA AKIRI KIWANGO CHAKE KUSHUKA ALIPOTUA MAN UNITED

Mlinda mlango wa Manchester United, AndreOnana amekiri kiwango chake kimeshuka tangu alipotua manchesterunited , lakini amewatoa hofu mashabiki kwa kueleza kuwa soon mambo yatakuwa sawa.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
20 Dec 2023
ONANA AKIRI KIWANGO CHAKE KUSHUKA ALIPOTUA MAN UNITED

Mcamerooni huyo, mwenye umri wa miaka 27, alitua Man United akitokea Inter Milan wakati wa dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, kama chaguo la kwanza baada ya David de Gea kuruhusiwa kuondoka bure kwenye kikosi hicho.

#Andre amekutana na wakati mgumu, akiruhusu mabao 39 katika mechi 25 alizochezea timu hiyo msimu huu, ikiwamo mabao 15 katika mechi sita tu za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa #Ulaya.

Baada ya kusemwa sana kuhusu kiwango chake, #Onana aliwajibu wanaomkosoa kwa kusema "kipa bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita ghafla tu amekuwa wa hovyo duniani.

"Kama nitazungumzia msimu wangu hadi sasa hapa #ManUnited, sifurahii kwa sababu ningeweza kufanya vizuri zaidi, najua naweza kufanya vizuri zaidi ya hiki kinachotokea sasa.

"Kila kitu ni cha kupita. Najua nitakuwa sawa. Kama sio leo, itakuwa kesho, kama si kesho basi itakuwa siku inayofuata baada ya kesho."

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.

YANGA SC KUTAFUTA MSHAMBULIAJI TISHIO DIRISHA DOGO.

YANGA SC KUTAFUTA MSHAMBULIAJI TISHIO DIRISHA DOGO.