

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imesajili zàidi ya Watanzania elfu tatu waliojitikeza kupata huduma kwenye maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara SabaSaba ambapo elfu mbili kati yao wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hapo hapo.
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imesajili zàidi ya Watanzania elfu tatu waliojitikeza kupata huduma kwenye maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara SabaSaba ambapo elfu mbili kati yao wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hapo hapo.
Hayo yamebainishwa July 9, 2023 jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi alipokuwa akishuhudia baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye banda hilo ambalo lipo kwenye Maonesho hayo yanayoendelea nchini.
"Tunatoa huduma zetu zote na tunaomba watanzania wazidi kujitokeza kwa wingi maana tumejipanga vizuri kuwahudumia watanzania,tunatoa vyeti hapa hapa kwenye maonesho na tayari wananchi zaidi ya elfu mbili tumewapatia vyeti na tunatarajia wazidi kujitokeza ili wasipitwe na fursa hii,” amesema Kanyusi.
Amesema jumuku la RITA ni kutoa huduma bora kwa wananchi wake hasa ikiwemo cheti cha kuzaliwa kupitia maonesho hayo, elimu kuhusu mirathi, kuandika na kuhifadhi wosia na wametumia nafasi hiyo kuwasaidia Watanzania waweze kusaidiwa kwa haraka kupata cheti na urahisi kupata cheti cha kuzaliwa.
Aidha baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma mbali mbali wamesifu utendaji kazi wa RITA na kusifu jitihada walizozifanya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa ndani ya siku moja.
"Tunawapongeza maana sio kazi rahisi kuwahudumia watu wengi kiasi hiki, hii inaonesha namna walivyojipanga vizuri mimi nimejiandikisha na nimepata cheti," amesema Leonard Cleopatra mmoja ya wananchi waliojitokeza kupata Huduma.
RITA inaendelea kutoa Huduma ya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa, elimu ya kuandika na kuhifadhi wosia kwenye Maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa hadi Julai 13, 2023.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU
MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI- DKT.SAMIA
BRELA Yawasogezea Huduma Wakazi wa Dodoma Wiki Ya Utumishi wa Umma.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
TANZANIA KUWA MWENYEJI TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII.