

Mchezo wa riadha umepeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa na kuipa Tanzania fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana ukanda wa Afrika Mashariki chini ya miaka 18 na 21 (EARR) ambapo Tanzania ilimaliza nafasi ya pili na tatu.
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO kwenye program ya Idara hiyo inayoendelea ya Wakuu wa Taasisi kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Taasisi za Serikali kwa miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Bi. Neema amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imeiongezea Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bajeti kutoka shilingi bilioni 35.44 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi shilingi bilioni 258 mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo bajeti hiyo imeirahisishia wizara na taasisi zake kutekeleza majukumu yake.
"Katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Rais Samia, sekta ya michezo nchini imepiga hatua kubwa ikiwa ni ishara ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza na kuendeleza michezo kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi", amesema Bi. Neema.
Ameongeza kuwa, Rais Samia ameleta mabadiliko ya kivitendo ambayo yameongeza ufadhili, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kisasa na ushirikiano wa kimataifa.
Katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo, Rais Samia amefanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa takriban shilingi Bilioni 31, ameanza ujenzi wa uwanja wa michezo Arusha utakaogharimu shilingi Bilioni 338 na Dodoma kwa shilingi Bilioni 310. Pia, anajenga viwanja vya mazoezi kwa gharama ya shilingi Bilioni 24.
Ametaja mafanikio mengine kuwa ni ; Tanzania kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo ya Kimataifa, kuondoa kodi kwa nyasi bandia, Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Tano na kuanzishwa kwa Mfuko wa Michezo.
Vile vile, Tanzania kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia, kuanzishwa kwa mfumo wa usajili wa Vyama na Vilabu wa kidijitali "SARS", kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa pamoja na timu za Tanzania kufuzu mashindano ya kimataifa.
Aidha Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika mchezo wa Kriketi mwaka 2024, imeweza kushinda mashindano ya ICC Mens T20 World Cup Sub Regional Africa Qualifier na kisha ikafanikiwa kushinda tena katika mashindano ya Mens ICC U 19 World Cup Qualifier Africa Division 2.
Kwa upande wa michezo ya watu wenye ulemavu nayo imekuwa ikiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa na kufanya vizuri ikiwemo katika mchezo wa tenesi wa viti mwendo na mpira wa miguu.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.