

Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watumishi wa Benki ya Azania ,Viongozi wa Shirikisho la Mpira nchini, Viongozi wa Klabu za Simba na Yanga, pamoja na wananchi mbalimbali wameshiriki kwenye Azania Benki Bunge Bonanza ambalo limeshirikisha Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga na kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Akizungumza katika bonanza hilo liliofanyika februari mosi,2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma Mhe.Majaliwa amesema Serikali imejipanga vyema kukamilisha maandalizi muhimu kwa ajili ya Michuano ya Mpira wa Miguu kwa Nchi za Africa CHAN na AFCON.
"Tanzania imejipanga vizuri, kuhakikisha kuwa michuano hii inafanyika hapa Nchini, Serikali inawajibika kuhakikisha inaandaa viwanja na miundombinu mingine."
Amesema kuwa tayari ukaguzi wa baadhi ya viwanja umefanyika na vimeonekana kukidhi vigezo “Viwanja vilivyokaguliwa vipo Tanzania bara na Visiwani, na kazi bado inaendelea, lengo ni kuhakikisha michuano hii inafanyika kwa ufanisi”
Amwongeza kuwa amesema ni vyema sasa Watanzania wakajipanga kutumia fursa zitakazo jitokeza kutokana na kuwepo kwa michuano hiyo hapa Nchini.
Aidha, ametoa Ponhezi Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa kuandaa Tamasha la Michezo la Bunge Bonanza ambalo limewakutanisha wabunge na wanamichezo mbalimbali wa Mkoani Dodoma.
Aidha ametoa Rai kwa Watanzania kuendelea na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Bonanza hilo lilianza kwa matembezi kutoka eneo la Chuo cha Mipango hadi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlini iliyopo Jijini Dodoma ambapo mashindano ya michezo mbalimbali kati ya Mashabiki wa Simba na Yanga yamefanyika.
"Kiukweli tumefurahi benki ya AZANIA kutuleta pamoja wanamichezo kwani inajenga undugu na kuimarisha afya zetu pamoja na kuhamasisha umuhimu wa mazoezi Kwa jamii ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa"Amesema Khadija Juma mmoja wa washiriki wa bonanza hilo ambaye ni shabiki wa Simba.
Naye Adam Peter ambaye ni shabiki wa yanga amesema kitendo walichokifanya AZANIA benki ni kitendo kizuri na Cha kuigwa na benki nyingine ikiwa ni kuhakikisha tunakuwa na jamii nzuriii inayopenda kulinda afya zao kupitia mazoezi.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.