

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro amezidi kumwaga Fedha za udhamini kwenye mashindano ya Ligi Daraja la Nne kwa miaka mitatu mfululizo katika Wilaya ya Ngara.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 17,2024 na Kamati Tendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ngara (NDFA) kwa kumpa pongezi na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Ngara NDAISABA GEORGE RUHORO kwa kuendelea kuwa Mdhamini Mkuu kwa miaka Mitatu mfululizo na kutoa fedha za Uendeshaji na zawadi mbalimbali za washindi wanaofanya vizuri katika Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Ngara.
Mwaka huu 2024 kwa Bingwa,Ruhoro ametoa Ng'ombe mmoja, Tsh 500,000 na Kombe, Kwa mshindi wa pili ametoa Ng'ombe mmoja na Tsh 300,000/= wakati Mshindi wa Tatu ametoa Ng'ombe mmoja na Tsh 200,000/= sambamba na mfungaji bora wa mashindano akipewa kiasi Tasilimu cha Tsh 20,000/=, Mchezaji Bora Tsh 20,000/=, Kipa bora Tsh 20,000/= na Timu yenye nidhamu Tsh 40,000/=
"NDFA tunaendelea kumshukuru kwa Ufadhili wake wa fedha za kuendesha Mashindano, Zawadi Tasilimu na Ng'ombe. Mhe. Ndaisaba George Ruhoro umeleta chachu ya kuimarisha na kuleta ushindani wa timu zaidi ya 16 zinazoshiriki Ligi yetu kila mwaka, kuibua vipaji Chipukizi
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI