REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000

Mkoa wa Njombe umeahidi kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia13,020 ili wananchi watumie nishati safi na salama.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
19 Nov 2024
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000

Hayo yamezungumzwa leo Novemba 19, 2024 na Kaimu Katibu Tawala,  Mha. Joseph Mutashubirwa baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA katika mkoa huo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Mha. Advera Mwijage mkoani Njombe.

"Nawapongeza REA kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, nishati hii ni salama na rafiki katika utunzaji wa mazingira yetu pamoja na afya za watumiaji wa nishati safi, " Amesema Mha. Mutashubirwa.

Aidha, Mha. Mutashubirwa ameihakikisha REA kuwa mkoa huo utatoa  ushirikiano na kuwahamasisha wananchi kuchukua mitungi ya gesi ya kupikia ili kuchochea uchumi na kutunza mazingira.

Kwa upande wake, Mha. Mwijage amezitaja wilaya zinazonufaika na mradi huo ni pamoja na Wilaya ya Njombe, Makete, Ludewa, na Wanging'ombe.

"Kila wilaya itasambaziwa mitungi ya gesi 3,255 ya kupikia kwa wananchi kupitia kampuni ya Taifa Gas. Tunaendelea kuhamasisha kujitokeza kwa wingi kuchukua mitungi hii inayotolewa kwa bei ya punguzo ya asilimia 50," Ameeleza Mha. Mwijage.

Ameongeza kuwa, elimu ya matumizi sahihi ya nishati safi inaendelea kutolewa kwa Watanzania ili kuhamasisha na kuchochea jamii kutumia nishati safi na salama.

SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO 2030 ASILIMIA 80% YA WATANZANIA WANATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP

WIZARA YA NISHATI IPO KWENYE MCHAKATO WA KUZALISHA MBOLEA KWA KUTUMIA GESI ASILIA.

WIZARA YA NISHATI IPO KWENYE MCHAKATO WA KUZALISHA MBOLEA KWA KUTUMIA GESI ASILIA.