Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa rai kwa wananchi kuacha kukopa kwenye taasisi zisizokuwa na leseni ya benki hiyo ili kukwepa kuumizwa na kutapeliwa pesa zao hasa katika kipindi hiki cha kuwa na taasisi nyingi za mikopo zinazofanya shughuli hizo mtandaoni.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa rai kwa wananchi kuacha kukopa kwenye taasisi zisizokuwa na leseni ya benki hiyo ili kukwepa kuumizwa na kutapeliwa pesa zao hasa katika kipindi hiki cha kuwa na taasisi nyingi za mikopo zinazofanya shughuli hizo mtandaoni.
Akizungumza Novemba, 14 2024 jijini Dar es Salaam kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha, Dickson Gama wakati akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa habari kuhusu usimamizi wa mikopo ya mitandaoni amesema ni jukumu la BoT kusimamia taasisi za fedha hivyo itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha shughuli za uchumi zinapatikana kwa wakati.
Amesema Banki Kuu imeandaa semina hiyo kwa wahariri na waandishi wa habari lengo ni kwajengea uelewa mzuri zaidi ili waweze kuelimisha umma.
"Ni jukumu la BoT katika kusimamia huduma Ndogo za fedha nchini hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kama kiunganishi kati ya Benki Kuu na jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla tunaamini kupitia mafunzo haya mtaenda kuelimisha umma na kujiepusha na mikopo ya kitapeli,"amesema.
Ameongeza kuwa semina hiyo ina umuhimu mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za utoaji mikopo mitandaoni pamoja na changamoto zake.
Gama amesema katika utekelezaji wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha ni jukumu lao kama wasimamizi wa sekta hiyo kuisimamia.
Ameeleza kuwa mikopo ya mitandaoni imekuwa ni sehemu ya mfumo wa fedha kwani imerahisisha utoaji wa huduma za mikopo kwa urahisi zaidi na haraka.
Amesema ukuaji huo wa haraka umesababisha changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya kimaadili, riba kubwa gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa.
Gama amesema kutokana na changamoto hizo wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili kufanya huduma hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi na mtoa huduma kuidhinishwa na BoT.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi idara ndogo za fedha Marry Ngasa amewataka watanzania kukopa kwa maendeleo lakini pia kuchukua hatua pindi taarifa zao zinapodukuliwa bila ridhaa zao kitendo kinachofanywa na wakopeshaji.
Aidha ameongeza kuwa BoT inaweka utaratibu wa kutoa taarifa kwa umma kupitia kurasa zao za mitandaoni kuhusu taasisi za mikopo zilizo na leseni ili kuwasaidia wananchi kuzitambua.
Sambamba na hayo Ngasa ameongeza kuwa zipo taasisi 55 ambapo wameshirikisha Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) ili kuzifungua kutoa huduma mtandaoni kwa kushindwa kukidhi vigezo.
"Kuna hatua mbalimbali ambazo tumezichukua ili kudhibiti athari za mikopo ya kidigital ikiwa ni pamoja kutoa elimu ya ukusanyaji wa madeni ambayo inalataza wazi wazi ukusanyaji wa madeni kwa kutumia lugha ya matusi,vitisho na kulipia hivyo tumeweka dawati la malalamiko hapa benki kuu ili kupoa malalamiko hayo pindi yanapojitokeza",Amesema Ngasa.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII