MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio lolote litakalotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kukutana kwa faragha kama walivyotangaza viongozi wa chama hicho, juzi.
Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda kujifungia kisha kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo ametoa angalizo jambo hilo ni lazima lifuate sharia za nchi.
Wasira amesema hayo leo alipohutubia wananchi katika mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani mjini Bunda.
“Wamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia mahali…ile ni honemoon.
“Tunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini tunawaambia lolote watakalotoka nalo kwenye honeymoon lazima lifuate sheria, waklija na honeymoon inavunja amani hatuwezi kuwaunga mkono.
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.