MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stiphen Wasira amepokelewa na Umoja wa wanawake wa CCM mkoa wa Dodoma huku akijinadi kuwa amepata nafasi hiyo kwa lengo la kuifanya CCM kuendeleza ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Urais,Ubunge na Udiwani.
Akizungumza na Umoja huo Wasira ambaye amepitishwa na mkutano mkuu wa CCM Taifa kwa nia ya kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Abdulrahman Kinana aliyejiuzuru nafasi hiyo.
Wasira amesema kuwa kazi kubwa ya chama hicho ni kuhakikisha inachukua dola kwa mara nyingine tena huku akiendelea kumpigia chapuo aliyepitishwa kugombea nafasi ya urais mwaka 2025 pamoja na mgombea mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi.
Wasira katika hotuba yake hakusita kurusha madongo kwa chama cha upinzani nchini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilichomaliza uchaguzi wake hivi karibuni wa kumpata Mwenyekiti,makamu mwenyekiti,katibu mkuu pamoja na wajumbe wake.
Hata hivyo Wasira ameesema kuwa wapinzani hawastahili kupewa nchi kwani wakipewa nchi kwenda Ikulu watagawana hata vikombe vilivyopo katika Ikulu hiyo.
"CCM itaendelea kushika dola na hakuna sababu ya kuwapa upinzani nchi ili waende Ikulu wakienda Ikulu watapigana na kugawana vikombe,wamefanya uchaguzi lakini wamekuwa na makundi na kugombana wao kwa wao sasa hao wanini kuwapa uongozi wa kwenda Ikulu"ameeleza Wasira.
Katika hatua nyingine amewataka makada na viongozi wote wa CCM kuachana na makundi na kuungana kwa nia ya kuifanya siasa safi ndani ya Chama na kutengeneza wepesi wa kuchukua dola.
"Natoa wito kwa viongozi wote wa CCM kuwataka kuachana na makundi na kutengeneza migogoro na kufanya chama kuwa kimbilio na kuachana na tabia ya kukaa maofisini na badala yake mnatakiwa kushuka kwa watu wa chini ili kujua hali zao"Ameeleza Wasira.
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.