WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

Wagombea nafasi ya ngazi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi kutambulishwa Kwa wanachama katika sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) zinazotarajiwa kufanyika tarehe tarehe 05 Februari mwaka huu.

Moreen Rojas (Dodoma)
By Moreen Rojas (Dodoma)
04 Feb 2025
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM  KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.

Hayo yameelezwa na  Katibu wa Itikadi na uenezi CPA Amosi Makala wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma na kusema kuwa jambo kubwa katika sherehe hizo zitakuwa ni jukumu kubwa la kuwatambulisha wagombea wa urais na makamu wa rais Tanzania bara na Tanzania Visiwani.

Chama hicho ambacho kinatimiza miaka 48 tangu kinaanzishwa kinatarajiwa kufanya sherehe zake katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa,sherehe hizo zitakuwa na viongozi mbalimbali ndani ya CCM na nje ya CCM.

"CCM inafanya sherehe yake ya kutimiza miaka 48 tangu kuzaliwa kwake na katika tukio hilo jambo kubwa ni kuwatangaza wagombea ambao walipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais na makamu ya Rais kwa Tanzania bara pamoja na mgombea Urais kwa Tanzania visiwani.

"Ijulikane kuwa kwa sasa CCM inawatangaza wagombea wao kwa wana CCM na muda ukifika watambulishwa kwa wananchi ili kufanikisha suala la kutimiza masuala ya uchaguzi kikatiba"Ameeleza Makala.

Aidha CPA  Makala amewataka wana CCM wote kutoka mikoa ya jirani na walioko katika Dodoma kuhakikisha wanafika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo .

"Napenda kuwaalika watanzania wote walioko Dodoma na nje ya Dodoma wana CCM na wasiokuwa wana CCM kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajili .

Aidha ameongeza kuwa CCM inapoadhimisha miaka 48 ni chama Imara na ndio chama kinachounda Serikali na kutekeleza miradi yake Kwa asilimia kubwa.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.

RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.

NIMEKUJA KUIKOMBOA CCM URAIS 2025; WASIRA

NIMEKUJA KUIKOMBOA CCM URAIS 2025; WASIRA

"TUMEAMUA KUSIMAMA NA LISU MBOWE AKAPUMZIKE"VIONGOZI CHADEMA WANENA

"TUMEAMUA KUSIMAMA NA LISU MBOWE AKAPUMZIKE"VIONGOZI CHADEMA WANENA