Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewafutia matokeo watahiniwa 67 waliofanya udanganyifu wakati wa mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka 2024 huku ikikifungia kituo cha mtihani chenye namba za usajili p6384 BSL Open School kilichopo mkoa wa Shinyanga kuwa kituo cha mitihani ya Taifa kutokana mipango ya udanganyifu.

Akitangaza matokeo hayo leo, Januari, 25 2025 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa NECTA,Dk. Said Mohamed amesema katika idadi hiyo wapo wanafunzi walioandika lugha ya matusi katika karatasi zao za mtihani wa kidato cha nne.
"Matokeo haya yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 (2) (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani mwaka 2016," amesema Dk. Mohamed.
Aidha ameongeza kuwa NECTA imezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 459 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2024 kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.
Amesema watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakufanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2025 kwa mujibu wa kifungu cha 32 (1) cha Kanuni za mtihani.
" kituo hiki kimefungwa kwa mujibu wa kifungu 4 (8) cha kanuni za mtihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa, " amesema
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.