TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

Dodoma.Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema Itajitahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara wote bila kuwa na upendeleo.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
17 Sep 2024
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

Hayo yameelezwa na Alfred Mregi kamishna wa kodi za ndani  wakati akizungumza na wafanya biashara katika kikao maalum kwenye ukumbi wa African dream jijini Dodoma.


Aidha amewaomba wafanyabiashara kutoa taarifa sahihi ili kuhakikisha hawatoi makadirio yasiyoendana na biashara zao.

Sambamba na hayo  ameongeza kuwa watafanya kazi kwa weledi wa kutosha kwani mbinu za wafanyabiashara zinabadilika kila siku

"Tutajitahidi kuwa na lugha ya staha(customer care) lakini kwa kutumia weledi wakati huo mkumbushe Afisa kutumia lugha ya staha,lakini mfanyabiashara unapokuja ofisini uje ukiwa na hali nzuri ya staha na sio kupaniki.

Aidha ameongeza kuwa wafanyabiashara wahakikishe wanakataa Rushwa kwani ni haki ya kila mtu kufuata sheria na sio kukiuka Maadili ya nchi hii.

" Asikudanganye mtu eti naweza kukufutia kodi yako wakati maafisa wengine wakipita unaanza kusema mwenzenu ashapita,hakikisha hautoi Rushwa ili kupita njia ya mkato hilo ni kosa kisheria"

Aidha pamoja na kwamba wanatoa elimu ni wajibu wao kama mamlaka kuwasimamia vyema wafanyabiashara kuwasilisha kodi kwa wakati na malipo yake.

Aidha amewapongeza wafanyabiashara kwa kuweza kulitumikia taifa lao na nimatumaini yao wataruka asilimia na kufikia malengo.

Kwa upande wake Mfanyabiashara Projest Hezron ametoa ushauri kwa mamlaka ya mapato TRA kutoa elimu kwa wafanyabiashara,kwani changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni kutokuwa na elimu ya biashara hivyo amewaomba mamlaka husika kutoa elimu pindi tu mfanyabiashara anavyoanza kufanya biashara ili apate uelewa mzuri.

"Angalieni namna gani yakuweza kuwasaidia wafanyabiashara wasifilisike kwani  biashara inazidi kukata mtaji kutokana na utitiri mwingi wa kodi ambazo tunalipa badala mtaji kuongezeka ndio tunazidi kufilisika,hivyo tunaomba muangalie kwa jicho la tatu suala zima la kodi"Amesema Mfanyabiashara James Lukas

Naye Anna John Mfanyabiashara na mjasiriamali ameiomba mamlaka kuwafikia wajasiriamali masokoni hususani kina mama kwani kumekuwa na usumbufu kwa wajasiriamali wadogowadogo na kuwapatia elimu sahihi ya ya umuhimu wa kulipa kodi na elimu hiyo iwe endelevu kwa kuzingatia haki na usawa kwa biashara husika.

Akitoa ushauri Gilbert Chuwa Mwenyekiti wa Jumuiya  wafanyabiashara Dodoma kwa niaba ya wafanyabiashara amesema kuwa wafanyabiashara wanafanya kazi nzurii kwenye taifa hili lakini kumekuwa na malalamiko ya wafanyabiashara kupata bili za milioni 5 na akilinganisha na biashara yake inakuwa sio sahihi hivyo amewaomba maafisa wa TRA kuangalia namna bora ya kuwaelewesha wafanyabiashara kwa kutoa mchanganuo mzuri ili mfanyabiashara aelewe na kulipa kodi anayostahili.

Aidha Chuwa amewasihi wafanyabiashara wa Dodoma kujiunga na Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania kwani ndio sehemu sahihi wanayoweza kuwasilisha mawazo yao na kuweza kupatiwa ufumbuzi kwenye ngazi ya kitaifa.

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA AGUSWA NA HUDUMA YA MALIPO KWA MKUPUO YA TTCL.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.

MWENYEKITI WA BODI YA T-PESA AWATAKA WANANCHI KUWA WAZALENDO.