Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja yaliyotokea usiku wa kuamkia jumatatu ya Septemba 16, 2024 Kata ya Nala Jijini Dodoma, Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimelaani tukio hilo na kutaka vyombo vya ulinzi na usalama kubaini chanzo cha mauaji hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk Anna Henga leo jumanne Septemba 17, 2024 taarifa hiyo imesema hivi karibuni kumekuwepo ongezeko kubwa la matukio ya kikatili nchini hususani ya mauaji, watu kupotea na kutekwa.
Taarifa hiyo imesema matukio hayo yanaongeza hofu kubwa kwa wananchi kwani yanatishia usalama wao na jamii nzima na kwamba ongezeko la matukio hayo pia kwa sehemu yanaashiria udhaifu wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi thabiti wa rai ana mali zao.
Kituo hicho kimetoa rai kwa mamlaka za ulinzi na usalama kuchunguza kwa kina tukio hilo ili kubaini chanzo cha mauaji hayo na kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa mujibu wa sheria za nchi.
Pia wamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi wa raia kwa kuchukua hatua za haraka na Madhubuti pindi matukio yanapotolewa taarifa ili kupunguza hali ya wananchi kuchukua sheria mkononi mwao na kuhakikisha raia wanalindwa na wanaishi kwa amani na usalama.
“Jamii nzima kuheshimu sheria na kuepuka kujichukulia sheria mkononi... badala ya kulipa visasi na kufanya matukio ya kikatili watafute suluhu za kisheria katika kutatua migogoro pia kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu matukio kama haya maana kujichukulia sheria mkononi ni kuzidisha matatizo na kuhatarisha amani katika jamii,” imesema taarifa hiyo.
Aidha viongozi wa dini na wa kijamii kuendelea kuhubiri amani na kuhamasisha umuhimu wa amani kutii sheria na kuzuia vitendo vya ukatili na kujichukulia sheria mkononi kwani vinakwenda kinyume na maadili ya jamii zetu, misingi ya Imani za dini n ani kinyumecha sheria.
“Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)kinasisitiza umuhimu wa kuendeleza utulivu, haki na usalama wa raia kwa kushirikiana na vyombo vya dol ana kuheshimu misingi ya haki za binadamu,” imesema taarifa hiyo
Dkt. Biteko asisitiza Tofauti ya Dini si Tatizo, Watanzania Waendelee Kuishi kwa Umoja na Amani
WANANCHI PAMOJA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAASWA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU.
TPDC YATOA IDHINI KWA TAASISI BINAFSI 40 UJENZI WA VITUO VYA CNG.
Halmshauri zashauriwa kuweka utaratibu bora kunusuru kaya maskini
TBA KUENDESHA OPERESHENI YA KUWAONDOA WADAIWA SUGU NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI.
Halmshauri zashauriwa kuweka utaratibu bora kunusuru kaya maskini
TBA KUENDESHA OPERESHENI YA KUWAONDOA WADAIWA SUGU NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI.
Dkt. Biteko asisitiza Tofauti ya Dini si Tatizo, Watanzania Waendelee Kuishi kwa Umoja na Amani
WANANCHI PAMOJA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAASWA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU.
TPDC YATOA IDHINI KWA TAASISI BINAFSI 40 UJENZI WA VITUO VYA CNG.