FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE KAPATA AJIRA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE KAPATA AJIRA.

Chuo cha ufundi stadi Furahika(VETA) wanatoa rai kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata elimu katika chuo hicho kwani asilimia 75 ya wahitimu wa chuo hicho wamepata ajira katika maeneo mbalimbali yakiwemo utalii na hotel.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
08 Sep 2024
FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE KAPATA AJIRA.

Chuo cha ufundi stadi Furahika(VETA) wanatoa rai kwa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata elimu katika chuo hicho kwani asilimia 75 ya wahitimu wa chuo hicho wamepata ajira katika maeneo mbalimbali yakiwemo utalii na hotel.

Pia,Chuo kinatarajia kufanya mahali Septemba 28 ili kuwaanga wanafunzi wanaombaliza na kuingia kwenye soko la ajira ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Septemba 7,2024 jijini Dar es salaam Kaimu Mkuu wa chuo Dkt David Msuya amesema wahitimu wanaotarajiwa kuagwa ni wale waliopo kwenye mfumo wa elimu bure ambayo inatolewa chuoni hapo.

"Wanafunzi wetu wanaohitimu ni wale waliokuwa kwenye mfumo wa elimu bure ambapo wanachangia kiasi cha shilingi 50000 tu kama gharama za mitihani yao ni hii inawezeshwa na serikali yetu lengo likiwa kugakikisha kila kijana nchini anapata ujuzi utakao msaidia kuondokana na utegemezi unaopelekea kuingia kwenye makundi maovu",Amesema Dkt Msuya.

Aidha amewataka wazazi kujitokeza kwenye mahafali hayo na kuwakaribisha wengine ili waje wajionee namna ambavyo vijana wanavyoweza kujikomba kiuchumi kwani wanapomaliza hapo wanauwezo wa kujiajili na kuajirika ambapo pia chuo kinachukua nafasi kubwa katika kuhakikisha vijana hao wanapata nafasi ya kufanyakazi katika taasisi mbalimbali kutokana na taaluma zao.

Sambamba na hayo Dkt Msuya amesema kuwa katika harakati wanazozifanya za kutokomeza ukatili wanatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo Zanzibar huku akitoa rai kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwafadhiri ili waweze kufikia lengo lao la kuhakikisha elimu ya ukatili inawafikia kila mtu hasa waliopo pembezoni.

Amesema wamekuwa wakijitolea kutoa elimu ya ukatili katika makundi ya watu mbalimbali hasa waliopo vijijini lakini changamoto kubwa inayowakwamisha ni jinsi ya kuwafikia wahusika kwani zaidi wanajiwezesha wenyeshe na kushirikiana na ofisi ya Maendeleo ya Jamii.

"Malengo yetu ni kuhakikisha elimu ya ukatili inawafikia wahusika wengi zaidi hasa waliopo vijijini kwa asilimia kubwa ndio waathirika wakubwa wa ukatili huo,lakini tunachangamoto nyingi zinazotukwamisha na ndio maana tunaomba wadau wajitokeze kutusaidia hata wakitupa gari hata kama ni bovu sisi tutarekebisha kwani litakuwa limetusaidia kuwafikia wahusika wetu",Amesema.

Pia,Dkt  Msuya ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaunga mkono lakini pia chama cha Mapinduzi CCM kwa kuendelea kuhakikisha watoto waliopo kwenye maeneo yao wanawapeleka chuoni hapo kupata elimu.

(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja

(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.