TAWA YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHANGARAWE WILAYANI MVOMERO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TAWA YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHANGARAWE WILAYANI MVOMERO.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Shillingi Millioni 5 (5,000,000) kwa Shule ya Msingi Changarawe iliyopo kata ya Mzumbe, Kijiji cha Changarawe wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
23 Jul 2024
TAWA YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHANGARAWE WILAYANI MVOMERO.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Shillingi Millioni 5 (5,000,000) kwa Shule ya Msingi Changarawe iliyopo kata ya Mzumbe, Kijiji cha Changarawe wilayani  Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Kamishna wa TAWA katika hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika Julai 22, 2024 wilayani humo, Kamanda wa Uhifadhi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Sylvester Mushy alimhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli kuwa TAWA itaendelea kushirikiana na wilaya yake kwa kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Aidha, Kamanda Mushy amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuitikia wito  wa kuhudhuria hafla ya kukabidhiwa madawati hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli ameishukuru  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mipango yake ya kuiwezesha Wilaya hiyo, pia ameipongeza TAWA kwa ufadhili walioutoa kwa wanafunzi wa Wilaya yake 

"Nichukue nafasi hii kuishukuru TAWA kwa uwepo wake katika Wilaya ya Mvomero kama wadau wa Uhifadhi, pia tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mipango yake ya kuiwezesha TAWA kifedha kwasababu imetusaidia sisi wananchi wa Mvomero kupata huduma ya madawati na vilevile kukabiliana na tatizo la wanyamapori wakali na waharibifu" amesema

Judith ameongeza kusema kuwa ufadhili wa madawati 60 uliotolewa na TAWA katika Shule ya  Msingi Changarawe utasaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo yao.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.