WANANCHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

WANANCHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

Kufuatia changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu nchini, wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani Shinyanga na Mwanza wamekubali na kuahidi kushirikiana na Serikali kukabiliana changamoto hiyo ili kupunguza adha kwa wananchi hasa wale wanaoishi pembezoni mwa hifadh

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
14 May 2024
WANANCHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

Kufuatia changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu nchini, wananchi wa  Mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani Shinyanga na Mwanza  wamekubali na kuahidi kushirikiana na Serikali kukabiliana changamoto hiyo ili kupunguza adha kwa wananchi hasa wale wanaoishi pembezoni mwa hifadhi.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania -TAWA katika Mikoa ya Kanda ya ziwa, wananchi hao wameelezea  adha  kubwa wanayoipata kutokana na changamoto itokanayo na wanyamapori  hao kiasi cha kuhatarisha maisha yao na kudhoofisha shughuli za kiuchumi huku wakiipongeza TAWA kwa hatua yao ya kuwashirikisha wananchi katika zoezi zima la kukabiliana na changamoto hiyo.

"Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kutokana na wimbi la wanyamapori hatarishi hususani fisi na wengine ambao wamekuwa wakishambulia watu, watoto wanashindwa hata kwenda shule, jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa" ameeleza Leonard Mayala mkazi wa Kahama

"Lakini ujio wa taasisi hii ya TAWA umekuwa ni faraja kubwa kwetu maana imekuja kwa ajili ya kushirikiana na wananchi ili kukabiliana na changamoto hii ya wanyamapori,..na mimi niseme, sisi kama wananchi tuko tayari kushirikiana na taasisi hii kwa sababu usalama ni wakwetu na taasisi hii imekuja na huu mpango kwa ajili ya kutuweka salama kwahiyo sisi wananchi tunaahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori hao" ameongeza

Naye Robert Wilson mkazi wa wilaya ya Misungwi Kata ya Mbarika ambaye pia  ni Mwenyekiti wa kikundi cha wagalu ameeleza kufurahishwa kwake na adhma ya Serikali kupitia TAWA ya kuwashirikisha wananchi katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika mapambano hayo ili jamii iwe na amani.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda amewapongeza wananchi hao kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo na kusema kuwa ushirikiano huo unatoa mwelekeo mzuri katika kutatua changamoto inayowakabili wananchi hao.

Katika kusisitiza hilo, amesema kutokana na ukubwa wa nchi yetu na upungufu wa rasilimali ni dhahiri kuwa TAWA peke yake haitaweza kuwepo kila mahali, hivyo ushiriki wa wananchi katika uhifadhi na mapambano dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu ni muhimu katika kufikia malengo mapana ya uhifadhi wa wanyamapori nchini, hivyo TAWA inathamini maamuzi yaliyofanywa na wananchi hao.

Aidha ametoa rai kwa watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ikizingatiwa kuwa jukumu la kulinda raia na mali zao ni la wananchi wote.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII