TFS YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU ZA MITI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

TFS YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU ZA MITI

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetakiwa kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za miche ya miti ili zifikie wananchi wengi zaidi na hatimaye kushiriki katika kuongoa misitu iliyotoweka.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
09 Jul 2024
TFS YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU ZA MITI

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  imetakiwa kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za miche ya miti ili zifikie  wananchi wengi zaidi na hatimaye kushiriki katika kuongoa misitu iliyotoweka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa ziara ya kikazi katika Kituo cha Uzalishaji mbegu za Miti leo Julai 9,2024  Mkoani Morogoro.

"Tuendelee kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mbegu na vyanzo vya mbegu na pia tuongeze Bajeti kukiwezesha kituo hiki" Mhe. Kairuki amesema.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amewataka kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na wahariri ili jamii ifahamu umuhimu wa mbegu bora za miti.

"Ni lazima muwe na maabara ya kisasa na pia mkitangaze kituo hiki kijulikane tuna mbegu za miche aina gani na tuna maabara" ameongeza.

Aidha, Mhe Kairuki ametilia mkazo suala la ukusanyaji maduhuli kujifanyia tahmini katika makusanyo na wanachotoa kwa Serikali.

Amewataka kutafuta  ushirikiano katika Taasisi nyingine Duniani kupitia  balozi  zilizopo nchini  lengo ikiwa ni kuongeza tija na mapato ya kituo hicho.

Kituo cha uzalishaji mbegu za Miti kiko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ambapo kinazalisha mbegu za miche ya matunda ya muda mfupi, miche ya mbao,kuni,kivuli, mapambo na miti ya kilimo mseto.

SEMFUKO AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA WANYAMAPORI.

SEMFUKO AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA WANYAMAPORI.

WAZIRI KAIRUKI AIPONGEZA TAWA KWA USIMAMIZI  MZURI WA RASILIMALI ZA WANYAMAPORI

WAZIRI KAIRUKI AIPONGEZA TAWA KWA USIMAMIZI MZURI WA RASILIMALI ZA WANYAMAPORI

WAZIRI KAIRUKI ATAKA WAZAZI KUTEMBELEA BANDA LA MALIASILI ILI KUZUNGUMZA NA WATAALAM WA VYUO VYA UTALII.

WAZIRI KAIRUKI ATAKA WAZAZI KUTEMBELEA BANDA LA MALIASILI ILI KUZUNGUMZA NA WATAALAM WA VYUO VYA UTALII.

DKT.ABASI :SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI KATIKA UTALII WA IKOLOJIA.

DKT.ABASI :SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI KATIKA UTALII WA IKOLOJIA.

TFS WAJA NA VIVUTIO SABASABA WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA FURSA ZITOKANAZO NA MISITU.

TFS WAJA NA VIVUTIO SABASABA WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA FURSA ZITOKANAZO NA MISITU.