TAWA YAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU UKEREWE | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

TAWA YAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU UKEREWE

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Joshua Bituri Manumbu ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa jitihada endelevu za kuelimisha jamii namna ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko na kuwadhibiti pale wanapoonekana kuhatarisha maisha ya wananchi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
09 May 2024

Pongezi hizo zimetolewa Mei 08, 2024 na Mwenyekiti huyo katika ziara iliyofanywa na Maofisa wa TAWA wilayani humo.

"Tumekuwa na matukio mbalimbali ya mamba na viboko kujeruhi watu lakini kupitia elimu inayotolewa na Maofisa hawa wa TAWA na namna wanavyowadhibiti, wameweza kuokoa baadhi ya watu lakini pia wameweza kuwaondoa wale wanyama ambao wameshafikia hatua mbaya ya kudhuru watu " amesema

Katika maelezo yake, Mwenyekiti huyo amesema Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Maofisa wa TAWA kutoka Kanda Maalumu ya Mwanza na imetoa ushirikiano mkubwa kwa Maofisa hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia Maofisa hao vitendea kazi  vinavyowafanya waweze kutekeleza majukumu yao kama sehemu ya taasisi muhimu nchini.

Kwa upande wao,  wananchi wa Kijiji cha Selema kilochopo Kata ya Bwiro wilayani humo wameipongeza na kuishukuru TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa wilayani humo ambayo wamekiri kuwa imekuwa msaada kwao na itawawezesha  kuendelea na shughuli zao za kiuchumi huku wakiepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori hao.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Selema wilayani humo,  Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amesema katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu Serikali inahakikisha usalama wa mwananchi unakuwa ni kipaumbele cha kwanza na ndiyo maana mara kwa mara Maofisa wa TAWA wamekuwepo maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu na kufanya doria katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa na changamoto ya wanyamapori hao.

Aidha Maganja ametoa wito kwa wananchi hao kuendelea kufanyia kazi maelekezo na elimu inayotolewa na wataalamu ili waendelee kuwa salama.

TANZANIA, NAMIBIA KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

TANZANIA, NAMIBIA KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

RC MAKONDA APONGEZA UONGOZI WA NCAA KWA MALENGO YA KUKUZA UTALII.

RC MAKONDA APONGEZA UONGOZI WA NCAA KWA MALENGO YA KUKUZA UTALII.

WANANCHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

WANANCHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

IDADI ya watalii walioingia nchini imetajwa kuongezeka  sawaa na Asilimia 27.2

IDADI ya watalii walioingia nchini imetajwa kuongezeka sawaa na Asilimia 27.2

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA WATEMBELEA MAKUYUNI WILDLIFE PARK.

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA WATEMBELEA MAKUYUNI WILDLIFE PARK.