DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu” | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

WANAWAKE mkoa wa Dodoma wamehamasishwa kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (Sacoss) kwani hilo ni suluhisho la mtaji litakalowaondole adha wanazopata kutokana na mikopo umiza au kausha damu Mwenyekiti wa Dodoma Women Sacoss (DOWOSA), Kitolina Kippa alisema hayo juzi wakati wa Mikutano mkuu wa tatu wa DOWOSA .

Mwandishi Wetu, DODOMA
By Mwandishi Wetu, DODOMA
14 Oct 2025
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

WANAWAKE mkoa wa Dodoma wamehamasishwa kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (Sacoss) kwani hilo ni suluhisho la mtaji litakalowaondole adha wanazopata  kutokana na mikopo umiza au kausha damu
Mwenyekiti wa Dodoma Women Sacoss (DOWOSA), Kitolina Kippa
alisema hayo juzi wakati wa Mikutano mkuu wa tatu wa DOWOSA .

Aliwataka wanawake kuendelea kuhamasishana ili waweze kujiunga na chama hicho kwani masharti yake ni nafuu ili waondokane na mikopo umiza na kausha damu.

Alisema kuwa riba ya nikopo ni asilimia moja tu.
Kippa alisema kuwa  Sacoss hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuwaleta na kuwaunganisha na kuwainua wanawake kiuchumi kwa kubuni mbinu na miradi mbalimbali itakayowasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi.

"Kuwaondolea wanawake adha waliyokuwa wanapata kutokana na mikopo umiza au kausha damu pale wanaposhindwa kulipa kutokana na mashartu kuwa magumu," alisema 
Pia kuwapatia mikopo wajasiriamali kwa riba nafuu na kwa urahisi,kuwapatia wanawake mafunzo mbalimbali yatakayowaongezea tija kwenye biashara zao.

Alisema kuwa kwa sasa kuna wanachama 580 kati ya hao walio hai ni 193 .
"Hawa ni wale ambao wamelipa kiingilio,wamenunua hisa 10 na kuweka akiba," alisema 
A'lisema kuwa wanachama sinzia wapo 387  ambao ni  wale ambao wengine walilipa kiingilio tu,wengine walilipa kiingilio na kununua hisa kidogo.

Alisema kuwa idadi ya hisa za wanachama hadi Septemba 2025 ni Sh milioni 23.9.
Alisema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa Septemba 2025 akiba za wanachama zimefikia Sh milioni 79.

Akizungumzia mkopo kwa wanachama alisema kuwa hadi Srptemba 2025,mikopo iliyotolewa ina thamani ya Sh 227.8 
Hata hivyo alitaja changamoto  mbalimbali ikiwemo wanawake wengi kutokuwa na mwamko wa kujiunga na Sacoss hiyo.

"Wanachama wengi waliojiunga hawapo hai kwa sababu hawajalipa hisa zinazotakiwa pamoja na kuweka akiba, pia baadhi ya wakopaji hawarejeshi mikopo kwa wakati na kusabanisha walipe adhabu," alisema

Aidha wakati mwingine mahitaji ya mkopo yanakuwa makubwa kuliko fedha ya Sacoss iliyokuwepo.

Mwenyekiti huyo  alisema kuwa wanatarajia kuongeza kiwango cha mkopo ili wakopaji wapate manufaa.
Alisema bodi inapendekeza kuongeza hisa kutoka 10 hadi 15 lengo kukuza mtaji wa chama.

Pia kuongeza kiwango cha kiingilio wanachama wapya watalipa kiingilio 50,000, hisa sh 150,000 na akiba Sh 100,000

Aidha alisema ifikapo Januari wale ambao hawajakamilisha hisa wataondolewa kwenye chama.

Alisema wanalenga kusiwe na mwanamke anayekaa nyumbani halafu aseme hajui cha kufanya.
"Hala tunalenga wafanya biashara ndogo ndogo waje asubuhi akafanye biashara kama ya kutembeza mboga na jioni arudishe Sh 11,000 kwani lengo letu ni kusaidia wanawake wainuke kiuchumi," alisema

Kwa upande wake,Meneja Benki ya Ushirika Tawi la Dodoma,Abdallah Salun alisema kuwa kama Benki wamekuwa wakitoa mikopo kwa Sacoss halafu Sacoss inakopesha wanachama wake.
"Sisi tunawapatia ukwasi na wao wanakopesha wanachama wao," alisema.

Naye mjumbe wa bodi wa Sacoss hiyo Mary Mabhaya alisema kuwa watafanya jitihada ikiwa ni pamoja ma kutoa elimu ili kuhakikisha wanawake wengi wanahamasika na kukiunga ili waweze kunufaika na mikopo yenye riba nafuu.

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

MKURANGA WAPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI

MKURANGA WAPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI

BAKWATA MWANZA YAWAHIMIZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA

BAKWATA MWANZA YAWAHIMIZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA

AMANI NDIYO UISLAMU, TUIHUBIRI NA KUILINDA- MUFTI ABUBAKAR

AMANI NDIYO UISLAMU, TUIHUBIRI NA KUILINDA- MUFTI ABUBAKAR