

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora Juma Mkomi amewasisitiza Watendaji Wakuu wa Taasisi na mashirika ya Umma kuendeIea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mifumo ya kielektroniki ya kusimamia utumishi wa Umma wa usimamizi wa Utendaji kazi (PEPMIS),na mfumo wa Usimamizi wa Utekelezaji wa Mradi (PIMS), kwa watumishi hao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora Juma Mkomi amewasisitiza
Watendaji Wakuu wa Taasisi na mashirika ya Umma kuendeIea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mifumo ya kielektroniki ya kusimamia utumishi wa Umma wa usimamizi wa Utendaji kazi (PEPMIS),na mfumo wa Usimamizi wa Utekelezaji wa Mradi (PIMS), kwa watumishi hao.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la nane la wafanyakazi Cha siku mbili amesema kuwa wafanyakazi watakao shindwa kutimiza takwa hilo hawata stahili kupandishwa vyeo huku akisema
mifumo hiyo ikitumika vizuri
utarahisisha utoaji wa huduma kwa wateja,wananchi.
"Najua ni mfumo mgeni wengi wetu hatuupendi unakuja kutubana lakini niwahamasishe kwamba mifumo hii imeletwa kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi.
Mkomi ameeleza kuwa uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi ni sehemu ya utekelezaji wa haki ya ushirikishwaji wafanyakazi na kufikia malengo ya kuboresha maslahi na mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi na waajiri katika maeneo yetu ya kazi.
Ameongeza kuwa uanzishwaji wa mabaraza hayo ni utekelezaji wa kifungu cha 74(1),(2) na (3), cha Sheria ya ajira na mahusiano kazini sura Namba 366 pamoja na kanuni 107 ya kanuni ya utumishi wa Umma za mwaka 2022.
Mkomi amefafanua kuwa uanzishwaji wa mabaraza hayo unatokana na matakwa ya kisheria kwa madhumuni ya kuishauri serikali, waajiri katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwamo usimamizi wa rasilimali watu.
"Baraza hili ni jukwaa muhimu mahali pa kazi kwani ni kiunganishi kati ya menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria na wafanyakazi waliopo katika Wizara hii.Ni matumaini yangu jukwaa hili litatumika kuishauri Wizara katika utekelezaji wa majukumu yake kusimamia maslahi, haki na ustawi wa wafanyakazi," amesema.
Kikao hicho ni maalum kwa ajili ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2024/2025 ambao pia ulenga kupima mafanikio ya shughuli za Wizara hiyo na kupata taarifa ya bajeti iliyopitishwa 2025/2026.
Akizungumzia uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanya Oktoba 29 mwaka huu amesema kuwa
"Mimi sina chama lakini ninamapenzi na watu fulani niwahamasishe watumishi wenzangu kwenda kushiriki kwenye uchaguzi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura," amesema.
Ameongeza kuwa wanasiasa kwenye mashujaa wanahamasisha watu kujitokeza kupiga kura na familia zao huku akiwaomba wajumbe wa baraza hilo ifikapo Oktoba 29 waende kupiga kura.
Akizungumzia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid alieleza kuwa anamini wajumbe wa baraza hilo watajadili namna ya kuboresha utendaji wa kitengo hicho huku akisema kitengo hicho kinakimbiliwa na watu huko mitaani wakiamini wanaenda kupata suluhu ya matatizo ambayo yao.
"Hivyo niwaombe wenzetu wanaosimamia kitengo hiki endeleeni kusimamia kwa ukaribu ili tuone matunda yanayitarajiwa kutoka kwenye kitengo hiki," amesema.
Awali Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi alisema kuwa lengo la baraza hilo ni kuwawezesha kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na utekelezaji wa mipango ya Wizara hiyo pamoja na changamoto ambazo wanakutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha
HAKUNA LITAKALOTOKEA OKTOBA 29, NENDENI MKAPIGE KURA- MSIGWA
TUKACHAGUE VIONGOZI TUWATAKAO KUEPUSHA LAWAMA NA MALALAMIKO
BADO TUNAMUHITAJI POLEPOLE KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
JAMII YAHIMIZWA KUWAKATAA WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA
CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA HUKU WAKIJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MIAKA 30