BAKWATA MWANZA YAWAHIMIZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

BAKWATA MWANZA YAWAHIMIZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA

Baraza la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limewaelekeza waumini wake kufunga kwa maombi kuanzia Alhamisi ya Oktoba 23, 2025 hadi siku yatakapotangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025 na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
12 Oct 2025
BAKWATA MWANZA YAWAHIMIZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA

Baraza la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limewaelekeza waumini wake  kufunga kwa maombi kuanzia Alhamisi ya Oktoba 23, 2025 hadi siku yatakapotangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025 na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

Akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza hilo Mkoa wa Mwanza Sheikh wa Mkoa huo wa Mwanza Hassan Kabeke amesema hatua hiyo inalenga kuiombea nchi amani na mshikamano, akisisitiza kuwa ni wajibu wa Kila Mtanzania kushiriki katika kuilinda amani hiyo ambayo imekuwa msingi wa maendeleo binafsi na ya Tanzania.

"Tarehe 23 Vituo vyetu vyote na misikiti yetu watafunga mpaka siku yatakapotangazwa matokeo. Ni maelekezo tumeyatoa. Hakuna kitu kigumu kama kukubali njaa lakini tutafunga kwaajili ya nchi hii kwani tunao wajibu wa kupigania amani ya nchi hii hasa kwa kurejea historia ya baadhi ya wazee wetu na wazee wa imani nyingine wameshiriki kuutafuta uhuru wa nchi hii." Amesema Sheikh Hassan Kabeke.

Kiongozi huyo pia wa imani amehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu ujao, akitaka Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya Vikao vya familia ili kukumbushana umuhimu wa kupiga kura sambamba na masuala mengine ya kijamii na kuachana na baadhi ya hamasa za maandamano na ulinzi wa kura vituoni unaotolewa na baadhi ya wanasiasa kwenye Mitandao ya kijamii.

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa dini amemtaja Dkt. Samia kama kiongozi hodari na aliyepokea nchi katika wakati ambao nchi iliandamwa na msiba na matatizo kadhaa ya kiuchumi, akiachiwa pia miradi mingi michanga iliyohitaji kuendelezwa, miradi ambayo sasa imekamilika na Taifa limeendelea kusalia tulivu, lenye amani pamoja na mshikamano.

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO