

Waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania kwa ujumla wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi hapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ili kupiga kura na kuwachagua Viongozi sahihi wanaoweza kuwaletea maendeleo sambamba na wote kuwajibika kuitunza amani ya Tanzania.
Waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania kwa ujumla wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi hapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ili kupiga kura na kuwachagua Viongozi sahihi wanaoweza kuwaletea maendeleo sambamba na wote kuwajibika kuitunza amani ya Tanzania.
Wito huo umetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ali Mbwawa wakati wa Mkutano maalumu wa viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu Mkoani Njombe, Mkutano uliofanyika Masjid Taqwa, Mwembetongwa Mjini Makambako, akisema amani ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa Taifa, akiwataka waumini wa dini hiyo kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha utulivu na mshikamano.
"Niwakumbushe kuwa Mtume wetu ni mtume wa amani, ni Mtume wa Kheri, Mtume wa baraka na ameitangaza amani amani hiyo kama alivyoitangaza Mungu. Niwakumbushe Vijana amani ndiyo jambo kubwa kuliko yote asije mtu hapa akawadanganya kwaajili ya kuondosha amani halafu wewe ukakubali. Muislamu kila jambo ukiambiwa fikiria ujue linafaa au halifai. Lindeni amani. Chungeni amani na kila mkipata hadhara simamemi semeni na hubirini kuhusu amani." Amesisitiza Mufti Abubakar.
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha
BADO TUNAMUHITAJI POLEPOLE KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
JAMII YAHIMIZWA KUWAKATAA WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA