

Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Dodoma imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa hatua kubwa ya kupunguza kero za kodi na ushuru kwa zaidi ya asilimia 85, hali ambayo imeleta nafuu katika biashara na kuongeza makusanyo ya mapato.
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Dodoma imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa hatua kubwa ya kupunguza kero za kodi na ushuru kwa zaidi ya asilimia 85, hali ambayo imeleta nafuu katika biashara na kuongeza makusanyo ya mapato.
Katibu Mtendaji wa jumuiya hiyo, Alexander Mallya, amesema wafanyabiashara sasa wanafanya kazi katika mazingira bora zaidi, tofauti na zamani ambapo changamoto za kodi zilikuwa kikwazo kikubwa.
Ameeleza kuwa jumla ya kero 119 zilizowasilishwa na wafanyabiashara, 109 zimepatiwa ufumbuzi na kubaki kero 18 pekee, huku 36 zikiwa katika hatua za mwisho za kumaliziwa.
Kwa mujibu wa Mallya, hatua hiyo ni ushahidi wa dhamira ya Rais Samia katika kujenga mazingira rafiki ya biashara na kuondoa urasimu uliokuwa unadumaza sekta hiyo.
Aidha, Mallya amesema wafanyabiashara wanatamani kushiriki kikamilifu kwenye sekta za kimkakati kama kilimo, madini na viwanda ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Amefafanua kuwa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa Dodoma ikiwemo reli ya kisasa ya SGR, Magufuli City, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato imefungua fursa kubwa za biashara, ajira na usafirishaji wa bidhaa.
Kwa upande wa mapato, amesema Dodoma imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo ya kodi baada ya kufikia zaidi ya shilingi bilioni 204 dhidi ya lengo la awali la shilingi bilioni 88 pekee.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yanaonyesha uaminifu wa wafanyabiashara kulipa kodi na mchango mkubwa wa serikali katika kurahisisha mifumo ya ukusanyaji.
Mallya pia amesisitiza kuwa serikali haiwezi kumtoza kodi kubwa mfanyabiashara mdogo, badala yake kila mmoja analipa kulingana na ukubwa wa biashara yake.
Ameeleza kuwa ulipaji wa kodi kwa hiari ndio msingi wa kujenga shule, hospitali, barabara na huduma nyingine za kijamii zinazowanufaisha wananchi wote.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma, Gilbert Chuwa, amepongeza serikali kwa kuondoa urasimu uliokuwa unaleta uadui kati ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Naye mfanyabiashara Sylivano James Chami amesema tofauti na zamani ambapo baadhi ya wafanyabiashara walilazimika kufunga maduka kutokana na madeni na changamoto za kodi, sasa mazingira yamekuwa salama na rafiki, hivyo amewataka wafanyabiashara wengine kulipa kodi kwa hiari na kuunga mkono jitihada za serikali ya Rais Samia.
"Kwakweli haya ni mabadiliko makubwa sana na tumepiga hatua nzurii na tunamshukuru Mhe.Rais Kwa kuchagua viongozi wazuri ambao ni wasaidizi wake wa TRA Kwakweli wanafanya kazi nzuri hakuna kero wala kufungiwa duka ni kujadiliana na Kila kitu kinakaa sawa"
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha
BADO TUNAMUHITAJI POLEPOLE KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
JAMII YAHIMIZWA KUWAKATAA WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA