WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE ZASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO DODOMA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE ZASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO DODOMA.

Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ambayo yameanza Tarehe 1 Agosti Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
02 Aug 2025
WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE ZASHIRIKI  MAONESHO YA KIMATAIFA  YA KILIMO DODOMA.

Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo  ambayo  yameanza Tarehe 1  Agosti Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma.

Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu iya " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025",

Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na   Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor  Mpango, Watalaam wa Wizara pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Nishati ikiwemo ukamilishaji wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na Usambazaji wa Umeme Vijijini, wanatoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia

Aidha wananchi wanafahamishwa kuhusu mipango mbalimbali ambayo Wizara imepanga kutekeleza katika mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kusambaza umeme vitongojini na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Taasisi za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA),  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)  Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania ( TGDC).

VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.

VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.

MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA*

BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA*

RAIS SAMIA ATOA BILIONI NNE UJENZI KIWANDA CHA KUZALISHA NISHATI MBADALA.

RAIS SAMIA ATOA BILIONI NNE UJENZI KIWANDA CHA KUZALISHA NISHATI MBADALA.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.