

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imevihimiza vyombo vya habari nchini kuripoti kwa usahihi na kwa wakati kuhusu taarifa zote zinazohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imevihimiza vyombo vya habari nchini kuripoti kwa usahihi na kwa wakati kuhusu taarifa zote zinazohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Kauli hiyo imetolewa leo, tarehe 1 Agosti 2025, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya Tume na Wahariri wa Vyombo vya Habari.
Jaji Mwambegele amesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya mpiga kura na taarifa sahihi zinazowawezesha kufanya maamuzi ya msingi kwa uhuru na kwa amani.
Aidha, amewasihi Wahariri wa vyombo vya habari kutumia majukwaa yao kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu, utakayofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Tume na vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia sheria za uchaguzi.
Akitoa mada kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani amesema vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kufanikisha maandalizi na uendeshaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ameongeza kuwa, katika nchi yoyote inayodhamiria kufanikisha jambo kubwa kama uchaguzi, vyombo vya habari ndio msingi wa kwanza, kwani kupitia kwao, wananchi hupata taarifa sahihi, zilizofanyiwa utafiti na kuhakikiwa.
Kailima amesema kuwa bila ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari, juhudi zote za Tume katika kutoa elimu na taarifa kwa umma haziwezi kuwafikia walengwa.
"Maana yake kila kinachotolewa na Tume hakiwezi kuwafikia wananchi iwapo vyombo vya habari havitaamua jambo hilo lifanikiwe," amesema.
Ameongeza kuwa wadau wote wa uchaguzi, vikiwemo vyama vya siasa, wanategemea vyombo vya habari kutoa taarifa zitakazowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Amesisitiza kuwa vyombo vya habari ndivyo vinavyoweza kuwa sauti ya kwanza ya kuonesha upotoshwaji wa aina yoyote unaofanywa kwa bahati mbaya au kwa makusudi kuhusu Tume na kuhusu zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
“Tunawaomba na kuwanasihi, kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi,” amesisitiza Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Aidha wahariri hao wamekumbushwa kutumia kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambayo ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura” kwenye taarifa zao wanazozitoa kwa umma ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji kwa wananchi kujitokeza kupiga kura.
Coop Bank Imejipanga Kutoa Huduma Maalum kwa Washiriki wa Maonesho ya NaneNane.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2025.
TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025