KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.

Katibu Mwenezi baraza la wanawake (BAVICHA)kutoka Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) amejiunga rasmi na CHAMA Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) baada ya kutoridhika na mwenendo wa chama chake.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
28 Jul 2025
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.

Katibu Mwenezi baraza la wanawake (BAWACHA)kutoka Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) amejiunga rasmi na CHAMA Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) baada ya kutoridhika na mwenendo wa chama chake.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ni muendelezo wa CHAUMA kuvunja ngome ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya leo Kada kindakindaki wa CDM kutoka mkoani Njombe, Sigrada Mligo kujiunga rasmi na chama hicho.

Tofauti hayo kada huyo ambaye kwa sasa ni mwanachama rasmi wa CHAUMA baada ya kukakibidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu, amesema ameamua kuondoka CHADEMA baada ya kudaiwa kutumika na anataka kukiua chama hicho alichokitumikia kwa jasho na damu tangu mwaka 2011 akiwa chuoni.

“Haikuwa kazi rahisi kufanya maamuzi haya, nimetafakari sana baada ya kupigwa na kuumizwa vibaya nje ya mkutano huku baadhi ya viongozi wakiaminika ndio waliopanga njama hizo na hatimaye kumtorosha mtuhumiwa.

“Pia hawakuhusika katika matibabu yangu hata kidogo, huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakachukua nafasi hiyo kwa kunikodishia gari ya wagonjwa na kunipatia Shilingi 1,500, 000 za matitabu ambazo baadhi nilizitumia kulipa deni la hoteli ambalo CHADEMA walikuwa wakidaiwa na baadhi nililipia gharama za matibabu.

 “CHADEMA nimekifanyia mengi ikiwemo ujenzi chama kwa fedha zangu, wageni wote wa chama waliokuwa wakifika Njombe,Mimi nilikuwa nawagharamia kila kitu lakini leo thamani yangu haionekani, natuhumiwa kukihujumu chama na kutaka kukiua sasa kabla hakijafa naamua kujiondoa ili maneno yao yasitimie nikiwepo, ukweli nimepoteza uhalali wa kuwa chadema kutokana na kauli hizo.

 “Pia nimefadhili operesheni mbalimbali cha kujenga chama kwa fedha zangu binafsi na nimetumia  zaidi ya         Sh. milioni 15 kuhakikisha majimbo matatu ya Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama na hakuna anayeweza kubisha kwani kumbukumbu zipo,” amasema. 

Hatua hiyo ya kujiengua CHADEMA kwa kada huyo inakuja miezi kadhaa baada ya kudaiwa  kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa Chadema wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti, John Heche, Machi 25, 2025, mkoani Njombe.

Katika mkutano alioufanya leo Julai 27, 2027 na Waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam Sigrada alifafanua kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita wa Chadema, alikiri kuwa kambi iliyomuangusha aliyekuywa Mwenyekiti, Freeman Mbowe kutokana na kuwepo kwa ahadi kedekede ambazo hadi sasa zimekuwa hewa na chama kuendeshwa kiharakati badala ya kimkakati.

Kulingana na hayo kwa sasa anamuomba aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe naye achukue maamuzi magumu kwa maana yaliyotarajiwa wakati wa uchaguzi si haya yanayoendelea sasa.

Sigrada kabla ya kujiunga CHAUMA, alikuwa ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Taifa (BAWACHA) ingawa pia alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali akiwa CHADEMA ikiwemo Udiwani Viti Maalumu.

TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.

TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.

CCM Yatangaza  Wagombea  Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.

CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.

VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025

VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025

INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.

INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.

INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UCHAGUZI KUTUMIA SHERIA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UCHAGUZI KUTUMIA SHERIA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.