SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.

SERIKALI imekiri kuwepo Kwa changamoto ya uendeshwaji wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka( UDRTS ) kwa awamu ya kwanza hivyo kwa kuliona hilo wameingia makubaliano na kampuni binafsi ya TRANSDAR kuanza kutoa huduma hiyo ili kuondoa hadha ya usafiri iliyopo sasa.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
24 Jul 2025
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.

SERIKALI imekiri kuwepo Kwa changamoto ya uendeshwaji wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka( UDRTS ) kwa awamu ya kwanza hivyo kwa kuliona hilo wameingia makubaliano na kampuni binafsi ya TRANSDAR kuanza kutoa huduma hiyo ili kuondoa hadha ya usafiri iliyopo sasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert chalamila mara baada ya kufanya ziara fupi ya  kutembelea miradi ya barabra inayojengwa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam amesema kuwepo kwa mabasi hayo 175 yatasaidi kuondoa changamoto hiyo kwa awamu ya kwanza kwanza ya mradi hivyo  changamoto hiyo itapungua au kumalizika kabisa baada ya mabasi hayo kuwasili.

"Barabara hizi zinaendelea kwa awamu ambapo jumla ya bilioni 613 zimetumika kwenye miradi hii ambapo kwa mradi wa awamu ya kwanza  awali kulikuwa na mabasi 200 ambayo yalikuwa yanatoa huduma kwa awamu hii ya kwanza na ndio maana wananchi walikuwa hawapati chamoto ya usafiri lakini sasa hivi magari yanayotoa huduma ni 60 pekee",Amesema.

Lakini kwa sasa mabasi yaliyobaki ni 60 hivyo serikali kwa kuona changamoto hiyo imeingia ubia na sekta binafsi kwa lengo la kuendesha mradi huo ambapo hivi karibuni kampuni ya trans dar itaingiza magari 175,"amesema.

Akizungumzia mradi wa awamu ya pili kutoka gerezani hadi Mbagala  Chalamila amesema wamepata  mwekezaji mwingine atakayeleta mabasi 200 kati ya hayo 99 yanatarajiwa kufika Agosti 15 mwaka huu na mengine 101 kuletwa nchini Septemba.

"Kwa kuzingatia uhitaji zaidi wa watu Mabasi yanayotarajiwa kufika nchini yatakuwa na urefu wa mita 18 na yatumia mfumo wa gesi tayari kama timu tulishaenda china kuyakagua ubora wake na tumejiridhisha yanafaa kutoa huduma nchini kwetu,"alisema.

Kwa upande wa mradi wa awamu ya tatu na ya nne ya  ujenzi unaendelea na ukikamilika tenda itatangazwa kwa lengo la kuwapata watoa  huduma kwenye njia hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) ,Dk.Athumani Kihamia amesema uwepo wa changamoto ya uchache wa mabasi ndio imeleta changamoto ya usafiri lakini kwa kuliona hilo tayari sekta binafsi zimeshajitokeza kuendesha mradi huo hivyo utasaidia kuondoa kero ya usafiri kwa mkoa wa Dar es salaam.

Aidha amewataka wamiliki wa mabasi ya daladala ambao wanatoa huduma katika maeneo yanayopita mradi wa mabasi yaendayo haraka wajisajili kama kampuni ili na wao waone namna ya kuwasaidia na kuwapatia maeneo mengine ya kutolea huduma hiyo.

Amesema tayari wameshazungumza na watoa huduma wapya pindi wanapoanza kutoa huduma hiyo wahakikishe kwa wakati wa asubuhi na jioni kila baada ya dakika tatu basi linakuwa kituoni kwani  muda huo wahitaji ni wengi.

MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.

MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.

SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.

SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.

DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.

DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA  KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.

DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.