

Mwakilishi wa mashujaa waliopigana vita vya kagera Balozi Brigedia Jenerali Francis Benard Mndolwa amesema anajivunia kuwa mmoja wa wapigania uhuru na kuwa mzalendo Kwa nchi yake na amewasihi wafanyakazi wote kuwa wazalendo.
Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya mashujaa tarehe 25 julai, 2025 katika uwanja wa mashujaa mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Hata nyinyi waandishi wa habari nawasihi kuwa wazalendo kwa kuandika habari zinakazowainua na kuwaheshimisha hivyo waandishi wa habari wote wanapaswa kuwa wazalendo kwani nchi hii inahitaji msaada wa Kila mmoja wetu"
Aidha amesema ili tuendelee kuwa na amani ni lazima kutanguliza uzalendo Kwani nchi nyingi zimeingia kwenye matatizo kwa kushindwa kulinda amani lakini Kwa hapa Tanzania Waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere na Karume wamefanya kazi kubwa sana.
"Tusiwe na mwenendo wa upinzani wa Dunia Kama warusi na china wanajaribu wakipambana lakini sisi hatuyataki hayo Umoja wetu Tanzania Bara na Tanzania Visiwani lazma tushirikiane kuilinda amani yetu"
Kwa upande wake mkazi wa Mtumba Bi.Leila Juma amesema anafurahia kuwa sehemu ya Kumbukumbu hii muhimu ya kuwaenzi mashujaa waliopigana Kwa ajili ya Taifa lao
"Nafurahi kuwa sehemu ya historia hii kiukweli nawapongeza mashujaa wetu kwani bila wao tusingekuwa hapa hivyo niwasihi watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu"Amesisitiza Bi.Leila
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.
MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.