WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME

Waziri wa nchi, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amezipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwa kusaidia kupunguza makali ya waliokuwa wateja wa FBME ambayo ilifungwa mwaka 2017.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
31 Jul 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME

Waziri wa nchi, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amezipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwa kusaidia kupunguza makali ya waliokuwa wateja wa FBME ambayo ilifungwa mwaka 2017.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS) wa BoT uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dk.philip Mpango Julai 30,2025 jijini Dar es Salaam. Dkt. Mkuya amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafarijika kwamba wateja wa FBME wameshalipwa asilimia 55 ya madai yao na kwamba jitihada za kupata fedha zaidi ili kuwarudishia zinaendelea.

“Kama mnavyofahamu, asilimia 60 ya wateja wa FBME nchini walikuwa kutoka Zanzibar na sasa tunafurahi kwamba asilimia 55 ya madai yao yameshapatikana na kwamba jitihada zinaendelea kupata fedha nyingine,” alisema Dkt. Mkuya katika pongezi zake kwa DIB na BoT katika zoezi hilo.

FBME ilifutiwa leseni yake na BoT mwaka 2017 na kukabidhiwa DIB kama mfilisi.

Ni katika ufilisi huo ambao unahusisha Tanzania na Cyprus ambako benki hiyo ilikuwa na tawi ndipo zimeweza kupatikana asilimia 55 za madai ya waliokuwa wateja wa FBME waliokuwa na zaidi ya kiasi kinachokingwa kilichokuwa kinatumika wakati huo cha shilingi 1,500,000.

Akizungumza hivi karibuni, Mkurugezi wa DIB, Bw. Isack Kihwili, alisema asilimi hizo 55, zilipatikana katika awamu mbili, awamu ya kwanza asilimia 30 sawa na shilingi Milioni 10,563.89, na awamu ya pili asilimia 25 sawa na shilingi milioni 8,991.75.

Hadi Mei 2025, kati ya wateja 1.414, jumla ya wateja 968 wamekwishalipwa fedha zao awamu ya kwanza kiasi cha shilingi Milioni 9,137.77, sawa na asilimia 86.5, huku waliolipwa awamu ya pili ya asilimia 25, wateja 960, ambao wamepokea shilingi Milioni 7,566.61 (sawa na asilimia 86.0 ya fedha iliyopatikana).

“Idadi ya wateja ambao hawajalipwa fidia ya ufilisi ya kiwango cha asilimia 30 kwa sababu mbalimbali hadi Mei 2025 ni 446, wenye jumla ya madai ya jumla ya shilingi Milioni 1,425.14,” alisema Bw. Kihwili.

Aidha, hadi mwezi Mei 2025, wateja 454 (sawa na asilimia 32) hawajalipwa fidia ya ufilisi ya kiwango cha asilimia 25 kwa sababu mbalimbali. Jumla ya madai yao ni Shilingi Milioni 1,235.81 (asilimia 14).

DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.

DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.

TBC KUAZIMISHA MIAKA 26 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KUENDESHA MASHINDANO YA INSHA KWA WANAFUNZI.

TBC KUAZIMISHA MIAKA 26 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KUENDESHA MASHINDANO YA INSHA KWA WANAFUNZI.

GAVANA TUTUBA: BENKI KUU ZIWE WASHIRIKA WA MAGEUZI YA KIUCHUMI

GAVANA TUTUBA: BENKI KUU ZIWE WASHIRIKA WA MAGEUZI YA KIUCHUMI

Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo

Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo