

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa rai kwa wasimamizi wa uchanguzi kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria katika kutekeleza majukumu yao ili kuufanya uchaguzi kuwa huru na wa haki.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa rai kwa wasimamizi wa uchanguzi kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria katika kutekeleza majukumu yao ili kuufanya uchaguzi kuwa huru na wa haki.
Wito huo umetolewa leo Julai 21,2025 na Mjumbe wa Tume hiyo, Balozi Omar Ramadhan Mapuri,wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo Mafunzo hayo yamejumuisha washiriki 106 na yanatarajiwa kumalizika Julai 23, 2025 huku yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo waratibu wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo pamoja na wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi.
Amesema kuwa utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi unapaswa kuongozwa na Katiba, sheria, kanuni na miongozo ya Tume.
"Katika kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi yanafanyika kwa kuzingatia misingi ya sheria, maadili, na utulivu ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wadau wa uchaguzi hivyo tunahitaji uchaguzi wenye amani, utulivu na unaoendeshwa kwa weledi wa hali ya juu. Hili linawezekana kama kila mmoja atasoma kwa kina na kuelewa nyaraka zote muhimu za uchaguzi, na kuuliza maswali pale panapotokea changamoto za uelewa,” amesema Balozi Mapuri.
Sambamba na hayo Balozi Mapuri amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanatambua mapema vituo vya kupigia kura ili kupanga mahitaji mahsusi ili kuhakikisha kuwa siku ya kupiga kura haina vurugu wala mkanganyiko bali inakuwa tulivu na yenye amani
Aidha meonya tabia ya upendeleo katika uteuzi wa watendaji wa vituo vya kupigia kura, akisisitiza kuwa waajiriwe watu wenye sifa zinazostahili ikiwemo wenye weledi, uzalendo, maadili na bidii ya kazi na si kuingiza watendaji kwa kigezo cha undugu au ujamaa.
"Niwaonye nyinyi ndio watendaji ambao mmeaminiwa na tume nendeni mkasimamie sheria lakini pia Tusiingize ndugu na jamaa wasio na sifa kwani Uchaguzi ni suala nyeti linalohitaji uadilifu wa hali ya juu,” amesema.
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.