TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imeendelea kutoa suluhisho la upatikanaji wa fedha kwa wakulima wadogo kupitia mikopo yenye dhamana nafuu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kubadilisha sekta ya kilimo nchini.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
01 Aug 2025
TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kitaifa Jijini Dodoma, Afisa Biashara wa TADB, Rosemary Gordon, amesema mfuko wa dhamana wa wakulima wadogo (SCGS) ulioanzishwa mwaka 2018 umewezesha wakulima 762,291 kupata mikopo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha.

“Changamoto ya dhamana imekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima,Mfuko huu unavunja kikwazo hicho kwa kushirikiana na taasisi za kifedha 19 kutoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi,” amesema Rosemary.

Rosemary ameongeza kuwa mfuko huo unatoa dhamana kwa mnyororo mzima wa thamani wa kilimo, ukisaidia wakulima kupata pembejeo, zana za kisasa za kilimo, pamoja na mikopo ya kuchakata na kuuza mazao,Zaidi ya shilingi bilioni 43.6 zimetolewa kwa dhamana ya ununuzi wa matrekta na vifaa vingine, huku bilioni 197 zikitumika kwa pembejeo.

"Tunatoa Mkopo katika mnyororo mzima wa thamani  kuanzia mkulima shambani mpaka mezani, mkopo wetu unawasaidia wakulima kupata pembejeo za kilimo Kama madawa viwatilifu ,mbegu,mbolea pia zinawasaidia kupata dhana za Kilimo kama matrekta,powertilers pia unawasaidia wakulima ambao wao wanachakata mazao mbalimbali na Kuna wale ambao wanauza na kununua mazao hao wote ni wamufaika wa Mfuko huu wa dhamana"Amesema Rosemary


Aidha amesema kuwa hawadili na wakulima pekee wanadili pia na wafugaji pamoja na wafugaji wa Kuku,Kuna wafugaji wa ng'ombe 
wa mziwa wanao nenepesha ng'ombe wote hao wananufaika na Mfuko huo wa dhamana.

"Na kwa hapa Tanzania Mfuko huu wa dhamana umeshafanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar kwahiyo tunapenda kuwakaribisha wale wote ambao wanakuja maeneo haya Kwa ajili ya maonyesho ya 88 mwaka huu wa 2025 hapa Dodoma waweze kufika kwenye Banda letu la Benki ya maendeleo ya Kilimo waweze kujifunza zaidi"Ameongeza Rosemary

Aidha awewasisitiza kina Mama pamoja na vijana katika kutoa dhamana,kwani Mfuko huo unatoa dhamana Hadi asilimia 70% na asilimia 50% mkopo ila Kwa upande wa vijana na wanawake Kuna ile miradi inayozingatia mambo ya climate smart wanatoa dhamana mpka asilimia 70%

Kwa upande wake, Afisa Biashara wa TADB Kanda ya Kati, Mariam Leonard, amesema benki hiyo inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima kuhusu huduma za kifedha zinazopatikana na fursa za mikopo ya moja kwa moja.

“Benki tayari imetoa zaidi ya shilingi trilioni 1.1 kwa wakulima na wadau wengine wa sekta ya kilimo. Tunataka kuona kila mkulima anapata nafasi ya kukuza shughuli zake kupitia mikopo na elimu tunayoitoa,” amesema Mariam.

TADB inafanya kazi na wakulima kote nchini, ikisisitiza ushiriki wa wanawake na vijana katika kilimo cha kibiashara, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuongeza tija na kuimarisha uchumi wa kilimo.

Maonesho ya Nanenane 2025 yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha wakulima na taasisi za kifedha, teknolojia na ubunifu, huku mfuko wa dhamana wa wakulima wadogo ukionekana kama chachu ya mageuzi ya kifedha kwa wakulima nchini.

Kauli mbiu ya Maonesho ya 88 mwaka huu  inasema "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025"

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.