BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA* | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA*

Benki ya Dunia (WB) imeeleza kuwa itatoa fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
23 Jul 2025
BENKI YA DUNIA KUJENGA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 400 KUTOKA UGANDA HADI TANZANIA*

*Yakutana na Mhandisi Mramba kueleza uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hauna athari kimazingira*

*Yaialika Wizara ya Nishati kushiriki Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York*

*Mramba aahidi kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia utekelezaji miradi ya Nishati*

Benki ya Dunia (WB) imeeleza kuwa itatoa fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha  umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.

Hayo, yameelezwa na Mtaalam wa Nishati kutoka Ofisi ya Benki ya Dunia nchini Tanzania, Dkt. Rhonda Jordan wakati alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba katika Ofisi za Wizara ya Nishati Mji wa Serikali Mtumba Julai, 23 Jijini Dodoma.

Dkt. Rhonda amesema kuwa kwa sasa benki hiyo imeridhia kutekeleza mradi huo baada ya kujiridhisha kuwa hauna athari za kimazingira kama ilivyokuwa ikielezwa hapo awali.

“Bodi ya Wakurugenzi sasa itapitisha fedha kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo, ambao ulikuwa ukisuasua kutekelezwa kwa madai ya kuathiri mazingira, lakini sasa bodi imeridhika na itatoa fedha za kuanza kuutekeleza”, amesema Dkt. Rhonda

Katika hatua nyingine, Dkt. Rhonda ameialika Wizara ya Nishati kushiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika Jijini New York nchini Marekani mwezi Semptemba, 2025.

Katika mazungumzo yao, Katibu Mkuu Mramba amemueleza Dkt.Rhonda kuwa wataendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo ule wa usafirishaji umeme wa Tanzania-Zambia (TAZA) na mingine inayofafana kama hiyo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga na Mhandisi Nishati Mkuu John Mageni.

VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.

VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.

MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

RAIS SAMIA ATOA BILIONI NNE UJENZI KIWANDA CHA KUZALISHA NISHATI MBADALA.

RAIS SAMIA ATOA BILIONI NNE UJENZI KIWANDA CHA KUZALISHA NISHATI MBADALA.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.

TAWOMA YATOA RAI KWA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KWENYE SEKTA YA MADINI.

TAWOMA YATOA RAI KWA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KWENYE SEKTA YA MADINI.