Uzalishaji Wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 18.21 Hadi Tani 27.43 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

Uzalishaji Wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 18.21 Hadi Tani 27.43

Mkoa wa Geita umeongeza uzalishaji wa madini kutoka tani 18.21 mwaka 2021 hadi tani 27.43 mwaka 2025 pamoja na uongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani 72,878,325.91 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani 92,204,527.35 mwaka 2025

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
21 Jul 2025
Uzalishaji Wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 18.21 Hadi Tani 27.43

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita tarehe 21 Julai 2025 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha Kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri yatokanayo na uchimbaji wa madini kutoka Shilingi  6,163,170,093.30 mwaka 2021 hadi Shilingi  10,582,192,189.88 mwaka 2025

"Kuongezeka kwa masoko ya madini kutoka masoko 10 mwaka 2021 hadi masoko 20 mwaka 2025, na Kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka leseni 903  mwaka 2021 hadi  9,774 mwaka 2025"Amesema

Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Afya ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya kutolea huduma za afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi.

Mafanikio hayo ni pamoja na:Kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Bukombe, Chato, Geita, Geita Manispaa, Mbogwe na Nyang’hwale;Kukamilika kwa ujenzi wa majengo matatu (3) ya huduma za dharura (EMD) katika Hospitali ya Bukombe, Katoro na Hospitali ya Halmashauri Nyang’hwale;Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Halmashauri ya Geita (Nzera) na ukarabati wa Hospitari ya Halmashauri ya Bukombe na  Manispaa ya Geita;Kuongezeka kwa idadi ya zahanati kutoka 129 mwaka 2021 hadi 198 mwaka 2025

Sanjari na Kuongezeka kwa vituo vya afya kutoka 25 mwaka 2021 hadi 42 mwaka 2025; Kuongezeka kwa nyumba za watumishi wa afya kutoka 180 mwaka 2021 hadi 230 mwaka 2025; Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka asilimia 80 mwaka 2021 hadi asilimia 90 mwaka 2025;Kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka 57 mwaka 2021 hadi vifo 55 mwaka 2025; naKupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka 5.1% mwaka 2021 hadi kufikia 4.90% mwaka 2025.

Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu yamewezesha kuongezeka kwa uandikishaji na udahili wa wanafunzi, ufaulu pamoja na kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata huduma ya elimu. Mafanikio hayo ni pamoja na:Kuendelea kutekeleza Mpango wa Elimu bila Ada kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita kwa kuongeza fedha za kugharamia mpango huo kutoka Shilingi 6,486,387,724.00/= mwaka 2021 hadi Shilingi 19,989,544,192/=mwaka 2025

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 Serikali ya awamu ya sita iliweka kipaumbele cha kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kaya nyingi zaidi zinaunganishwa na huduma ya maji.

Serikali ya awamu ya sita  imeendelea kutekeleza shughuli za kilimo katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kilimo kinakuwa chenye tija na usalama wa chakula unaimarika.

Serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa sekta ndogo ya Mifugo kama shughuli kuu ya kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa. Kutokana na umuhimu huo, Serikali ya Mkoa wa Geita katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 had 2025 imeendelea kuhimiza ufugaji wa kisasa wenye kuzingatia kinga, tiba na utafiti wa mifugo ili ufugaji uweze kuwanufaisha wananchi.

Sekta ya nishati imeendelea kuwa mhimili muhimu katika kuwezesha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Geita. Kutokana na hilo, CCM iliisimamia Serikali katika kuhakikisha kuwa Mkoa unakuwa na nishati ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi na kijamii.

Serikali inatambua kuwa sekta ya michezo na sanaa ina umuhimu mkubwa katika kutoa burudani, kuelimisha jamii, kuimarisha afya, kuunganisha jamii, kuzalisha ajira na kudumisha mila, tamaduni na desturi za kitanzania.

Serikali imeendelea kutilia mkazo umuhimu wa maendeleo ya wananchi pamoja na ushirikishwaji wa makundi maalum ikiwemo vijana, wanawake na Watu Wenye Ulemavu ili kuleta usawa wa kijamii na kiuchumi kwa wote.

Hali ya Uchumi ya Mkoa imeendelea kuimarika ambapo Pato halisi lilikua kutoka Shilingi 7,031,590,000/= mwaka 2021 hadi Shilingi 9,122,637,000/= mwaka 2024 sawa na ukuaji wa asilimia 31 Vilevile, pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi 2,769,308/= mwaka 2021 hadi shilingi 2,814,714/= mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 1.6.

Hali ya ulinzi na usalama  katika Mkoa imeendelea kuwa  shwari  kutokana na ushirikiano uliopo baina ya vyombo vya Dola na Wananchi. Hali hii imewawezesha wananchi kuishi kwa amani na utulivu na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi, kijamii na kisiasa

Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46

Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46

Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90

Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90

UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA NJIA YA KISASA UMEONGEZEKA.

UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA NJIA YA KISASA UMEONGEZEKA.

Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5

Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*