

Kufuatia ongezeko la watalii nchini, uliochagizwa na Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Mkoa umepokea Kiasi cha shilingi Bilioni 103 kwa ajili ya uboreshaji wa Viwanja vya Ndege viwili, Uwanja wa Ndege Arusha eneo la Kisongo na Uwanja wa Ndege ziwa Manyara, kiasi hicho cha fedha kimefanya maboresho ili kuvipa hadhi na kuonheza idadi abiria kufuatia idadi ya miruko.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Kenani Laban Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita tarehe 20 Julai 2025 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma
Aidha amesema kuwa Kiasi hicho Cha fedha kimetumika Kuboresha eneo la maegesho ya magari kiasi cha Shilingi milioni 640 na shilingi Bilioni 2.8 zimetumika kujenga Jengo la kisasa la abiria pamoja na kuongeza barabra za kurukia ndage. Ujenzi umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa abiria.
"Uwanja huu wa ndege ni wa pili kwa miruko ya ndage Tanzania na watatu kwa idadi ya abiria ikifuatia Kilimanjaro International Air port na Julias Nyerere International Air Port, hata hivyo Serikali imetoa shilingi bilioni 11 kwaajili ya kutengeneza mindombinu ya taa ndani za kuongozea ndege, kukamilika kwa matengenezo hayo utaanza kufanya kazi kwa saa 24 na kupokea ndege za kimataifa"Amesema
Aidha Shilingi Bilioni 88.539 zimetumika kuboresha Kiwanja cha Ndege Ziwa Manyara huku Bilioni 5.93 zimetumika kulipa fidia kwa Waathirika 187, Mradi ambao utasaidia kufikia malengo ya utalii katika ukanda wa Kaskazini ukiwemo Mkoa wa Arusha.
"Utalii ni Sekta muhimu ambayo inamgusa Kila mtu Hadi mwananchi wa kawaida mfano madereva waongoza Utalii,wahudumu wa hoteli ambapo hapa hata mama mboga atauza mboga zake hotelini na kujipatia kipato hivyo Sekta ya Utalii Kwa Mkoa wetu inagusa watu wote mpka mwananchi wa chini kabisa anajipatia kipato na kujikwamua kiuchumi"Amesisitiza
Kupitia Mamlaka ya Uhifadhi Ngorongoro Mkoa unatekeleza Mradi wa ujenzi wa Jengo la Makumbusho ya Jiolojia ya kisasa, (NGORONGORO - LENGAI UNESCO GLOBAL GEOPARK) linalojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya China, kwa gharama ya shilingi Bilioni 25.
"Jengo hilo ni maktaba ya inayoonesha mandhari ya vituo vyote vinavyopatikana ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro Crater pamoja na Jamii zote zilizowahi kuishi ndani ya bonde hilo la Ngorongoro, lengo likiwa ni kulinda na kutangaza urithi wa Jiolojia na utamaduni ndani ya Hifadhi pamoja, kuongeza maudhui ya kielimu kupitia muundo wa makumbusho yenye taarifa za kisayansi, Kuboresha huduma kwa wageni pamoja na kuongeza muda wa kukaa wageni na kuchochea uchumi wa maeneo ndani ya Mkoa"Ameongeza
Sanjari na hayo Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwekeza kwenye sekta ya michezo ikiwa na lengo la kuimarisha sekta ya utalii, Serikali imetoa shilingi Bilioni 298 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa SAMIA SULUHU AFCON ARUSHA, ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya AFCON mwaka 2027 yanayotarajia kufanyika nchini, ujenzi umefikia 44.2%
Katika Sekta ya Miundombinu ya Barabara, Mkoa wa Arusha umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 635.8 kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja.
Katika Sekta ya Killimo na ikiwa ni kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa, na kwa Mkoa wa Arusha asilimia 75 ya wakazi wake wanategemea shughuli za kilimo na ufugaji, Mkoa umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 85.2 kwa ajili ya sekta ya kilimo na shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Mifugo.
Aidha, Mkoa umepokea jumla ya shilingi Bilioni 57.22 kutoka kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF). Kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 38.39 kwa ajili ya uhawilishaji wa fedha kwenye kaya masikini na shilingi Bilioni 18.82 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu.
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye kasi kubwa ya maendeleo. Wananchi wa Arusha wanashuhudia mapinduzi ya maendeleo katika sekta zote. Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya sita, chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkoa wa Arusha umejikita katika kuboresha miundombinu katika Sekta za Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya Barabara, Nishati, Kilimo & Mifugo, Utalii pamoja na Utawala Bora.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.