

Katika kipindi cha 2020 hadi 2025, Mkoa wa Kigoma umeendelea kunufaika na uwekezaji wa Serikali katika kukuza utalii, ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya kitalii kama vile Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Hifadhi ya Taifa ya Mahale, Ziwa Tanganyika pamoja na vivutio vya kihistoria na kiutamaduni kama Kituo cha kumbukumbu ya Dk. Livingstonekilichopo Ujiji.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita tarehe 19 Julai katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Watalii wa ndani wameongezeka kutoka 630mwaka 2020 hadi 11,769mwaka 2025,Pia, Watalii wa nje wameongezeka kutoka 345mwaka 2020 hadi 655kufikia mwaka 2025.
Aidha Sekta ya madini ina nafasi ya kipekee katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni na ukuaji wa uchumi kwa ujumla, Mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa sekta hii ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa dhahabu kutoka gramu Elfu 12.5 mwaka 2020 hadi gramu Elfu 15.2 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 22
"Kuongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa Dola za Marekani Elfu115.4 mwaka 2025 sawa na madini kutoka Dola za Marekani Elfu 22.6 mwaka 2020 hadi ongezeko la asilimia 411"
"Kuongezeka kwa masoko ya madini kutoka SokoMoja (01)ni Soko la zamani la Madini Kakonko na Soko jipya la Madinimwaka 2020 hadi masoko Mawili (02) mwaka 2025 ambayo la Kigoma; na Kuongezeka kwa utoaji wa leseni za uchimbaji kutoka leseni 354 mwaka 2020 hadi leseni 799 mwaka 2025"Ameongeza
Katika Sekta ya Maliasili na Utalii Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuendeleza na endelevu wa huduma za kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa kuhakikisha uhifadhi mzuri wa maliasili sambamba na upatikanaji jamii.
Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, Mkoa 141,yenye jumla ya hekta 91,691katika Halmashuri zote za umefanikiwa kufanya hifadhi endelevu kwa misitu ya Vijiji Wilaya pamoja na Usimamizi wa misitu ya halmashauri 3 za Uvinza(Msitu wa Masito na Lyabutongwe) na Kasulu (Msitu wa Makingi) zenye ukubwa wa hekta 208,556.
"Uendelezaji wa misitu13ya hifadhi ya Serikali Kuu yenye ukubwa wa hekta 222,919na Usimamizi wa kitalu kimoja cha uwindaji chenye ukubwa wa Hekta 100,000 kinachoitwa Makere-Uvinza Open Area Hunting Block,Uendelezaji wa Hifadhi za Nyuki ambapo jumla ya misitu 7 ya Vijiji imetengwa na kuwa hifadhi za nyuki katika Wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu"
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imefanikiwa kuingia mkataba wa kuuza hewa ya ukaa katika Msitu wa Masito
"Kufanyika kwa ugawaji wa ardhi kwa matumizi ya kilimo na ufugaji kwa wananchi, ambapo jumla ya hekta 10,000 zilitolewa kutoka kwenye Msitu wa Makere Kusini na kugawiwa kwa Kijiji cha Mvinza (hekta 2,174), Kijiji cha Kagerankanda (hekta 2,496)na Halmashauri (hekta 5,342)kwa ajili ya wakazi wengine kwa shughuli za maendeleo"
Kwa kushirikiana na wadau wa mazingira Mkoa umeendeleza kampeni za upandaji miti ambapo kuanzia 2020hadi kufikia mwaka 2025, jumla ya miti Milioni 34.5 imepandwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kigoma,Lengo ni kuongeza uoto wa asili, kuhifadhi vyanzo vya maji, na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.