

Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makalla ametangaza kuwa chama hicho kimejipangia tarehe ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wake kwa nafasi za Ubunge na Udiwani kuwa ni tarehe 28, mwaka 2025.
Makalla, amewataka wagombea wote wa nafasi za Ubunge na Udiwani kuwa wavumilivu na watulivu kwani kikao cha maamuzi kitafanyika Julai 28,2025
Amesema kikao hicho ndicho kitatoa maamuzi ya mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea watakaopitishwa na kuelekea hatua ya kura za maoni, kwa mujibu wa ratiba rasmi ya chama.
“Wagombea wote wa ubunge na udiwani waendelee kuwa watulivu. Tunajua kuna hamasa na matarajio makubwa, lakini chama kinafanya kazi kwa umakini na kwa kuzingatia taratibu zote. Kikao cha maamuzi ni tarehe 28 Julai, na kutoka hapo tutaelekea kwenye kura za maoni,” amesema Makalla.
"Idadi ya wagombea ni kubwa, hivyo chama kinachukua muda kufanya uchambuzi wa kina ili kuhakikisha kila mmoja anatendewa haki kwa mujibu wa vigezo na kanuni,” ameongeza.
"Chama chetu ni makini. Hatufanyi kazi kwa pupa. Tunataka kuhakikisha tunapata wagombea bora watakaoleta ushindi na maendeleo kwa wananchi,” amesema.
Amesema Mchakato huo wa uteuzi unaelekea katika hatua muhimu, ambapo wagombea waliopitishwa watachuana kwenye kura za maoni, kabla ya majina yao kuwasilishwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Aidha ameeleza kutakuwepo na kikao cha Halmashauri kuu ya taifa 26 kitakachofanyika jijini Dodoma ambacho kitatanguliwa na kakao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa .
CPA Makala pia alisisitiza kuwa chama kinasimamia mchakato huu kwa uwazi, umakini na haki, na kwamba hakuna mgombea atakayeachwa bila kuangaliwa kwa umakini.
Aidha, alieleza kuwa kikao hicho kitaanza kwa kikao cha Kamati Kuu, ambacho kitakuwa sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea uteuzi rasmi, kabla ya kuanza kwa mchakato wa kampeni ndani ya chama.
Amesema chama hicho kimeamua kuongeza muda ili kuhakikisha kila hatua ya uchambuzi inafanyika kwa makini na kwa kuzingatia vigezo, huku akiwataka wagombea kuwa watulivu wakati mchakato huo ukiendelea.
“Wagombea watulie, wa relax wakati tunaendelea na mchakato mpaka tarehe 28” amesisitiza.
Mchakato huu ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, ambapo CCM kama chama tawala kinaendelea na hatua mbalimbali za kuwapata wagombea wake bora kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi mbalimbali.
Makalla amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuhairishwa kwa kikao ambacho kingefanya uteuzi tarehe 19 Julai Mwaka huu Jijini Dodoma.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.