

Watu kadhaa wameripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa nchini Syria kufuatia mashambulizi 10 ya anga yaliofanywa na Jeshi la Israel (IDF) katika mji wa Dara kabla ya alfajiri ya kuamkia leo
Al Jazeera, imeripoti leo Alhamisi Aprili 3,2025, kuwa masahambulizi hayo yaliofanywa na Israel yalilenga katika eneo la msitu wa Jubailiyah lilipo katika mashamba yanayopatikana katika mji wa Daraa magharibi mwa Syria.
Haya yanajiri siku moja baada ya mashambulizi mengine kulenga uwanja wa ndege wa Hama, uwanja wa ndege wa Damascus, na kwenye mashamba yaliyopo mji wa Homs.
Hata hivyo Mapema siku ya Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ilitangaza kuwa Israel ilifanya mashambulizi ya anga katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Hama na kuuharibu na kuwajeruhi raia na wanajeshi.
Vyanzo vya kijeshi vya Syria viliiambia Al Jazeera kwamba ndege za kivita za Israel zililipua jengo la utafiti wa kisayansi katika kitongoji cha Masaken Barzeh mjini Damascus.
Vyanzo hivyo pia Viliongeza kuwa ndege za Israel zililenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa T4 katika jangwa la Homs linalopatikana katikati mwa taaifa la Syria.
Hata hivyo mashambulizi hayo pia yameripotiwa kusababisha majeraha kwa baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo la uawanja huo.
Sambamba na hayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ilisema kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel ni jaribio la wazi la kurejesha hali ya kawaida ya ghasia ndani ya nchi hiyo, na kwamba kwa Israel sio haki na ni jaribio la makusudi la kuiyumbisha Syria na kurefusha mateso ya watu wake.
Lakini pia Wizara hiyo imelaani uchokozi huo na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, pamoja na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Israel kusitisha uchokozi wake na kutii sheria za kimataifa.
Kwa miezi kadhaa, Israel imekuwa ikianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Syria karibu kila siku, na kuua raia na kuharibu maeneo ya jeshi la Syria.
Israel ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Syria kwa miaka mingi wakati wa utawala wa Rais aliyepinduliwa Bashar al-Assad, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhusiano baina ya vituo vya kijeshi vya Iran ambavyo vinatajwa kama sehemu ya kuunga mkono kundi la Hezbollah Lebanon.
Vita hivi pia vinaripotiwa kuanza Tangu 1967, baada ya Israeli kuchukua sehemu kubwa ya Milima ya Golan. Lakini pia matumizi mabaya ya hali ya Syria kufuatia kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.