DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ametoa wiki moja kwa uongozi wa TANESCO kufanya maboresho ya Kituo cha huduma kwa wateja na matokeo yake yawe wazi kwa Wananchi lakini pia ameagiza kufumuliwa kwa Kituo hicho kufuatia kituo kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa viwango vinavyotarajiwa.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
09 Jan 2025
DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko  ametoa wiki moja kwa uongozi wa TANESCO kufanya maboresho ya Kituo cha huduma kwa wateja na matokeo yake yawe wazi kwa Wananchi lakini pia ameagiza kufumuliwa kwa Kituo hicho  kufuatia kituo kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa viwango vinavyotarajiwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo Januari 9,2025 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea kituo hicho pamoja na mambo mengine lakini pia kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Aprili, 2024.

Dkt. Biteko ameshangazwa na hatua ya TANESCO kuweka kando maelekezo yake ya mwezi Aprili 2024 yaliyolitaka Shirika hilo kuondokana na  matumizi ya namba za kulipia kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (free toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ili kuwapa unafuu wananchi wanaohitaji huduma za TANESCO.

" Wewe ulishapiga simu, pesa yako ikakatwa na huduma usiipate? Wananchi wanaumia sana!" naagiza kuundwa upya kituo ili kuongeza ufanisi na tija kwa Wananchi, "kituo hiki kinategemewa na Watanzania wengi na huduma inayotolewa hapa hairidhishi kabisa," amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Rais Samia imetoa fedha nyingi kuhudumia kituo hicho lakini utendaji wake ni mbovu kuliko huduma ya kituo.

TANESCO ilielekezwa kuachana na matumizi ya namba za kulipia Kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA ili kuwapa unafuu wa Wananchi wanapopiga kuhitaji huduma za TANESCO.

Akizungumzia utendaji wa Kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Abubakar Issa amesema kulikuwa na changamoto za kibajeti. Hivyo ameahidi  kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA watakaa haraka na kuanza matumizi ya namba bila malipo ili kutoa unafuu kwa wananchi na kuleta tija kwa watumiaji.

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.

MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.

MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.

ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA.

ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA.

WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO

WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO

WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENIĀ  YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA

WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENIĀ  YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA