

Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda ametoa taarifa kwa umma juu ya kusogezwa mbele kwa tukio la uzinduzi wa Sera ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 na mitaala iliyoboreshwa kuwa rasmi tukio hilo litafanyika mapema Februari mosi mwaka huu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 januari 2025,kwenye ofisi za Wizara ya elimu zilizopo jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa anawasihi wageni ambao tayari wamekwisha anza safari waje dodoma na watapata siku Moja ya kulijua vizuri Jiji la Dodoma huku wakisubiri tukio hilo na Kwa wale ambao bado hawajaanza basi waangalie namna ya kuendana na mabadiliko.
"Tuna jua wapo walioanza safari za kuja tunaomba watuvumilie na wabaki Dodoma na ambao bado hawajaanza waweke vizuri ratiba zao ili kuenda sawa na tarehe hiyo"
Aidha tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu lilipagwa kufanyika tarehe 31,januari mwaka huu na sasa limepelekwa mbele kwa sababu zisizozuilika amabapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo utahusisha wadau wa elimu mbalimbali kutoka Tanzania bara na Visiwani kwani ni jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa Kwa hamu na wadau wa Sekta ya elimu ili kujipambanua Kitaifa na kimataifa.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.