Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini Godfrey Kimario amesema wameamua kusimama na Tundu Lisu ili kufanya mabadiliko ya Siasa za Uimara.
Kimario ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na Viongozi wa Chama hicho wanaomsapoti Tundu Lisu Kwa asilimia 100% na wenye kiu ya kutaka mabadiliko makubwa katika chama chao.
Aidha ameongeza kuwa ni wakati wa Freeman Alikaeli Mbowe kumuachia kijiti Cha Mwenyekiti Tundu Lisu kwani Mbowe ameshapoteza mvuto wa kisiasa na hana maono mapya yanayoendana na kasi ya chama chao.
"Tukimpata Tundu Lisu chama chetu kitakuwa Imara kwani hivi Sasa Mbowe amekuwa legelege na hayupo sawasawa na kasi ambayo sisi tunaihitaji kama chama,tunahitaji mabadiliko katika taifa letu"Amesema Mwenezi
Kwa upande wake Mwenyekiti Wilaya ya Dodoma Mjini Stephen Karashan amesema wanahitaji mabadiliko ili wanachama wa Chama hicho waendelee kukiamini chama hicho na sio Kwa maneno bali Kwa vitendo.
"Ni wakati wa Freeman Mbowe kupumzika na kuwa mshauri Mkuu wa Chama hiki kwani ni wazi amekijenga chama hichi lakini ni wakati wake wa kupumzika na kumuachia Tundu Lisu ambaye ataenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye chama hiki"
"Mtu anatoa hela milioni 250 ili asujudiwe jambo ambalo sio sawaa kwani hatuwezi kufika popote kwani watanzania wanasema mkituletea mgombea yuleyule hakutakuwa na mabadiliko katika chama hiki kwani hatuhitaji kuwa watumwa wa mtu Kwa kuwa na kiongozi anaetumia fedha"
Aidha amesema amechukizwa na kitendo Cha Makamu Mwenyekiti CCM Stephen Wasira kumuombea kura Mbowe jambo ambalo limeonyesha dhahiri sio mzalendo na akitaka usalama katika hili akatae kauli ya Wasira kwa kujiengua kwenye uchaguzi.
"Sisi Viongozi wa Dodoma tunaondoka hapa na tunatoa Rai kwamba hatutaki kufuatwa fuatwa,hatuhitaji kupokelewa wala kutafutiwa hoteli sisi tunakwenda kufanya haki na kubwa zaidi nasisitiza Mbowe ajiondoe kwenye uchaguzi"
Aidha ameongeza kuwa ikitokea Mbowe akashinda wao kama Viongozi wa Dodoma watakuwa na maamuzi magumu kwani majimbo yote 10 yanamsapoti Lisu.
WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU
BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.
MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.
JK AIPA PPAA CHANGAMOTO KUOKOA FEDHA ZA SERIKALI KATIKA MIRADI
ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AZINDUA KAMPENI YA 'USIKU KAMA MCHANA'KWENYE WILAYA HIYO.
UKATILI WA KIJINSIA,MIGOGORO YA ARDHI NA NDOA ZATAJWA KUWA CHANGAMOTO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI.
ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AZINDUA KAMPENI YA 'USIKU KAMA MCHANA'KWENYE WILAYA HIYO.
NIDA YATOA RAI KWA WANANCHI KUPELEKA VITAMBULISHO VYENYE CHANGAMOTO ILI WAPATIWE VITAMBULISHO VIPYA
WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENIĀ YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA
WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO