

Wagombea nafasi ya ngazi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi kutambulishwa Kwa wanachama katika sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) zinazotarajiwa kufanyika tarehe tarehe 05 Februari mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Itikadi na uenezi CPA Amosi Makala wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma na kusema kuwa jambo kubwa katika sherehe hizo zitakuwa ni jukumu kubwa la kuwatambulisha wagombea wa urais na makamu wa rais Tanzania bara na Tanzania Visiwani.
Chama hicho ambacho kinatimiza miaka 48 tangu kinaanzishwa kinatarajiwa kufanya sherehe zake katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa,sherehe hizo zitakuwa na viongozi mbalimbali ndani ya CCM na nje ya CCM.
"CCM inafanya sherehe yake ya kutimiza miaka 48 tangu kuzaliwa kwake na katika tukio hilo jambo kubwa ni kuwatangaza wagombea ambao walipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais na makamu ya Rais kwa Tanzania bara pamoja na mgombea Urais kwa Tanzania visiwani.
"Ijulikane kuwa kwa sasa CCM inawatangaza wagombea wao kwa wana CCM na muda ukifika watambulishwa kwa wananchi ili kufanikisha suala la kutimiza masuala ya uchaguzi kikatiba"Ameeleza Makala.
Aidha CPA Makala amewataka wana CCM wote kutoka mikoa ya jirani na walioko katika Dodoma kuhakikisha wanafika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo .
"Napenda kuwaalika watanzania wote walioko Dodoma na nje ya Dodoma wana CCM na wasiokuwa wana CCM kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajili .
Aidha ameongeza kuwa CCM inapoadhimisha miaka 48 ni chama Imara na ndio chama kinachounda Serikali na kutekeleza miradi yake Kwa asilimia kubwa.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.