Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Watumishi wa Umma waaswa kuwa na nidhamu kazini na kuacha kutumia madaraka vibaya pamoja na kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo kwa namna yeyote ile.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
19 Dec 2024
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Hayo yameelezwa na Deus Sangu Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati akifunga Kikao kazi Cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa Jiji Mtumba jijini Dodoma.


Aidha amewataka maafisa utumishi kuangalia vijana wanaoingia kwenye ajira Kwa kuwafundisha maadili na sio kuwafundisha mambo yasiyofaa ikiwemo Rushwa na mikopo umiza.

Aidha amesema kuwa anachukizwa na kitendo Cha waajiri kuwa na lugha mbaya huku wengine wakiendekeza Rushwa ya fedha kwa ambao wanakuwa wamepata ajira mpya kazini na kuwaambia kuwa ili kufanikisha jambo ni mpka atoe Rushwa kitendo ambacho sio sawaa na ni kinyume na maadili.

"Rushwa ya ngono imekuwa kikwazo kikubwa ambapo zaidi ya wafanyakazi wa kike 30 wametoa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo Kwa mtumishi mmoja wa kiume kuwaomba Rushwa ya ngono ili waweze kusalia kazini"


Kwa upande  wake Katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Selemani Mkomi amesema  katika majadiliano yaliyofanyika katika kikao hicho imebainika kuwa bado kuna changamoto katika masuala ya Utawala wa wasimaminzi wa rasilimaliwatu katila utumishi wa umma hususani katika eneo LA kutafisri sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia watumishi wa Umma.

" Changamoto kubwa imejionyesha katika eneo la kushughulikiaji wa mashauri ya kinidhamu kutozielewa sheria kanuni taratibu na miongozo na usimaminzi hivyo washiriki wamesisitizwa kuendelea kuzisoma sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia utumishi wa umma ili kuendelea kubobea katika maeneo Yao ya utawala, "

Kikao kazi hicho kimebeba kauli mbiu isemayo"Kusimamia Sera na Sheria za Utumishi wa Umma kupitia Mifumo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Kidijitali iliyoboreshwa"

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano  katika tukio la kariakoo.

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano katika tukio la kariakoo.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.

JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.

FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU

FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU