Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe.Balozi Thobias Makoba amesema anawashukuru sana waandishi wa habari kwa kipindi alichofanya kazi pamoja na kwa ushirikiano, ambapo amesema wamekuwa wazalendo katika utekelezaji wa majukumu yao akitolea mfano wa namna ya kukesha pamoja kwenye tukio la ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo.
Balozi Thobias ameyasema hayo leo desemba 13,2024 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.
Aidha ameishukuru Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kwa kufanya kazi pamoja kwa ushirikiano kuanzia viongozi wote hadi wafanyakazi wa ngazi zote.
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa amesema anaamini atafanya kazi kwa kukidhi matumaini na matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amempa nafasi ya kulitumikia taifa.
"Nawashukuru sana waandishi wa habari wenzangu kwa namna mnavyofanya kazi yenu ya habari kwa nguvu na weledi, naomba tuendelee kushirikiana"
"Nawashukuru viongozi wanaoondoka wanaoniachia kijiti kwa kazi kubwa waliyoifanya, Idara ya Habari - MAELEZO niliyoiacha ni tofauti na ninayoikuta, naahidi na naamini tutasonga mbele zaidi"
Aidha amesema Baada ya Sikukuu za mwisho wa mwaka, atakutana na waandishi wa habari ili kujipanga jinsi atakavyofanya kazi ili tusonge mbele kwa maslahi ya nchi, kwani kazi yetu sisi waandishi wa habari ni kuilinda Tanzania kwa kalamu zetu.
Aidha ameongeza kuwa Tarehe 19 Desemba, 2024 Jijini Dar es Salaam, atakuwa na taarifa ya kwanza ya Msemaji Mkuu wa Serikali na atazungumza mengi siku hiyo yanayohusu maendeleo ya taifa letu.
"Waandishi wa habari tuungane kwa pamoja kuwapa Watanzania taarifa za nchi yetu"
"Nimeambiwa baadhi ya masuala mbalimbali ya waandishi wa habari yanayohitaji kufanyiwa kazi, naahidi kuyashughulikia kwa nguvu kubwa,ninachoomba ni ushirikiano wenu"Amesisitiza Msigwa.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Nicholaus Mkapa amesema Kwa niaba ya uongozi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, anatoa shukurani kwa viongozi na wafanyakazi wa Idara ya Habari - MAELEZO kwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika ujenzi wa Taifa katika kipindi chote walichokuwa pamoja.
"Tunaikabidhi Idara ya Habari - MAELEZO kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo sasa ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa na Taasisi zake tatu ambazo ni Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), na Bodi ya Ithibati"
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO
DAR CITY YAING’ARISHA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU AFRIKA MASHARIKI
Watumishi wa Umma Waaswa kujifunza mifumo mipya ya Tehama ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
DAR CITY YAING’ARISHA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU AFRIKA MASHARIKI
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.